Uzi wa kupeana connection za pamba kali

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
10,805
Reaction score
14,181
Kuna pamba unaziona mtu kavaa town unajiuliza hivi wanazitoa wapi? Mfano mimi natafuta full jeans nyeusi nimeulizia nimeshindwa ukiingia ebay manguo mabayaaaa, huwa naopti mtumba grade 1 nawapa madogo wa pale Karume ofa nzuri wapambane.

Pia natafuta leather trouser nyeusi na brown na mapigo yangu ya kunatishia ila wapi unapata ya kishamba hebu tuibiane maujuzi watanashati wasafi.

Hii nimeipata juzi kwa grade one pale Karume kwa jofuu.

 
Leteni machimbo wakuu vijana wangare..
 
Hapa sibanduki mpaka mtaje tshirts v collar plain za mtumba size M .Sitakuja kuvaa tshirt ambayo sio V maisha yangu yote yaliyobakia duniani .Nimeichoka midabwada ya kichina.
 
Nenda pale Morroco kuna jamaa anaitwa Ustaadh, yupo karibu na ile saloon ya yule mzee wa vikao (Aristote). Jamaa ana vitu classic sana sema bei tu imeshiba kidogo. Na siku moja moja unajikunja unaingia Woolworth pale mzee baba naamoni utapata nguo nzuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…