Vyanzo vya taarifa vinaeleza kuwa chanzo cha FUNDI MAIKO ni kutoka katika mkoa ambao haujatajwa ambapo fundi mmoja aliyefahamika kwa Jina la Maiko alipewa kazi na halmashauri moja (naifadhi jina lake) kuandika kibao cha uzinduzi wa jiwe la msingi katika moja ya shule ya msingi(inaifadhiwa jina) ili iweze kuzinduliwa na mbio za mwenge.
Hata hivyo fundi maiko hakulipwa ujira wake mpaka mwenge unakaribia kufika eneo hilo alikuwa hajalipwa fedha zake.
Aliamua kuandika kibao kinachoeleza aliyekitengeneza na kueleza madai yake ikiwa ni shinikizo kwa wakimbiza mwenge kulipwa fedha zake.(tazama picha ya kwanza,unaweza kujua halmashauri husika).
Tangu hapo ndipo lilipoanza kuibuka jina la fundi maiko.