Uzi wa kuweka picha zilizotengenezwa na kompyuta

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Habarini wakuu
Nimeamua kuanzisha huu uzi maalumu kwa kuweka picha zilizotengenezwa kwa mifumo ya kompyuta. huu utakuwa ni uzi wa kuweka picha tulizozitengeneza sisi wenyewe na si picha za ku download au kuweka picha kutoka kwa mtu mwingine.

Huu uzi ni wa kujumuisha watu wote: wanaozalisha animations au still pictures, wanaofanya kama hobby au wanaofanya kama profession yao, wanaojifunza na waliobobea. Lengo ni ku share kazi zetu, kurekebishana ili tuweze kuboresha ujuzi wetu katika eneo hili. Ni vema pia ukiweka picha ukatoa maelezo madogo kama software uliyotumia kutengeneza picha hiyo, vitu au mbinu uliyotumia hadi ukapata picha ya aina hiyo. Siyo lazima kutoa maelezo hayo ila itakuwa ni vizuri kwa kuwa unaweza kuwa msaada kwa watu wengine.
Asanteni

Chumba cha habari

Hii ni moja kazi za hivi karibuni, niliitengeneza juzi. Nimetengeneza kwa kutumia blender, na kazi zangu zote ninatumia blender. Hiyo picha niliyoiweka kwenye screen niliichukua jamiiforums kipindi flani cha nyuma kutoka katika uzi wa wapiga picha na nikawa naitumia kama background kwenye pc yangu, credits kwa aliyeipiga. Hivyo nikaamua niiweka kwenye screen hapo ili kuongeza ka mvuto kidogo. Inaonekana vyema japo bado kuna mengi ya kurekebisha.

Uko tayari? Just a joke



Sijui niliwaza nini hadi nikatengeneza hii kitu.


DNA

Kama ushawahi kuangalia video ya wimbo wa uitwao DNA wa Kendrick Lamar nahisi utakuwa unaifahamu hii set. Hapo nilikuwa najaribu kuchallenge uwezo wangu kwenye swala la mwanga. Bado mambo si mazuri sana japo inafanania kiasi Fulani.

Can you spot me there?



Old project

Hii ni moja ya kazi nilizozitengeneza mwanzoni kabisa najifunza hii softwere. If you know tha building.


Je unaweza taja sehemu zote kama ulivyokuwa shule ya upili?


Nipo, nitakuwa napandisha picha kadri nitakavyokuwa najaaliwa na kuzitengeneza.

kama unayo yako, shiriki nasi.
 
Mkuu software ipi nzuri ya kuchora watu napenda kuchora wanawake wenye mizambwanda
ipo moja ninayoifahamu mimi inaitwa makehuman. inakuja na sample ya binadamu halafu wewe unakuwa unabadilisha values katika maeneo mbalimbali ili upate matokeo unayoyataka. ila kama unataka kuzama deep sana ni vema kujifunza kutengeneza mwenyewe kwa sababu ukiizoea itakulemaza. but kama kwa matumizi ya kawaida ni nzuri sana, kama misabwanda utatengeneza msambwanda wa saizi inayokukonga moyo wako kabisa.
 
Huwa natamani hayo madude ila mambo ya Software yamenipitia kushoto.
 
GETO LA MSELA


this is the one of craziest render i ever made. nilitumia masaa kama kumi na moja kuikamilisha. japo sakafu kama imenizingua hivi lakini ni moja ya picha inayonivutia kwa kweli. nafikiri nitahitaji kuongeza mijusi mijusi hapo ukutani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…