Kama sikosei umesema wastani wa siku mbili/tatu si ndio?
Hapo bajeti itakuwa kipengere mkuu, labda kwa kujibana mnoo na usitake makuu ππ.
Ngoja tuanze kubreak down.....300k Tsh.
- Nauli kwenda/kurudi , π’ daraja la kawaida- 35k x 2 = 70k
- Accommodation π - Hapa ndio mtiti sana, kwa zanzibar kupata malazi kwa bei nafuu ni issue hasa kipindi cha high season ambapo wageni wanakuwa ni wengi sana, nashauri kwa bajeti hiyo muda mzuri ni wa low season, kipindi hiki ni kizuri tena ni vema ukatumia applications kama airbnb, booking.com kufilter accommodation kutokana na bajeti yako. Nimeattach baadhi ya accommodation zenye bei nafuu kwa kipindi cha low season kutoka airbnb na booking.com.Hapa tuweke bajeti kuanzia 45k (Tsh) per night x 2= 90k laki ishakata hapo ππ
N.B: Mitandao mingine ya kupata malazi ya bei nafuu ni pamoja na agoda, homestay, hostelwords n.k hizi wenzetu wazungu wanatumia sana hasa wale solo travellers, packpackers na wasafiri wengine wa bajeti nafuu.
- Chakula π²π₯π₯- Hapa nitakuachia wewe mwenyewe kutokana na ulaji wako. Ila naamini huwezi kumaliza laki kwa siku mbili/tatu.
Kama utakuwa stone town muda wa jioni utahitaji kwenda forodhani kupata misosi, gharama za usafiri ni kama bara, boda boda ya kukutoa hotelini na kukurudisha kama accommodation itakuwa mbali. Mimi mara nyingi huwa kuna chimbo langu lipo karibu na bandarini nikifika S.town lazima nilale hapo na sihitaji usafiri kufika sehemu nyingi, ni mwendo wa "andha kanoon" tu kukata mitaa ya mji mkongwe kwa miguu.
Sasa mpaka hapo tumeshaona malazi na usafiri ushagharimu karibia laki na 80, bado hujala, hujanunua zawadi kwaajili yako na uwapendao (not important though) ila kuna jambo la msingi hupaswi kulikosa uwapo S.town. si jingine bali ni....
- Excursions- Ukiacha kutembealea maeneo kama Old slave market kwaajili ya kuona historia ya biashara ya utumwa, kukatisa mitaa ya stone town kujionea mandhari mazuri ya magofu ya kale, ngome kongwe na vivutio vingine vinavyopatikana katikati ya mji ambavyo vingi havina gharama Ni vyema ukatenga kiasi cha pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio kadhaa ambapo utahitajika kuwa na kiasi fulani cha pesa.
- A day trip to (Changuu) "Prison Island" & "Nakupenda beach" -Changuu/ Prison island kisiwa kidogo kilichojitenga, utapata kujua historia yake lakini pia utaweza kujionea kobe wakubwa wenye umri mpaka miaka 200 wanaopatikana hapo, vile vile utaweza kwenda kutembelea beach nzuri ya "nakupenda" kama ni mpenzi wa snorkeling basi hapa ni mahala pake, packae huhusisha chakula (sea food plata, viazi mbatata mkaango, matunda na soft drinks) kabla hujamaaliza trip yako.
Hapa kwa mTZ si chini ya elfu 80K Tsh kama utashare usafiri (boat) na wenzako.
Mpaka hapo utakuwa umepata mwanga wa bajeti kiasi gani utapaswa kuandaa, NB: Hii ni breakdown ya kujibana sana (budget) ila ukitaka makuu ya kwenda kulala 5 star hotel, Boat First class chakula 3 courses kazi kwakoππ .
Nina imani nitakuwa nimekupa ABCs za kutosha kwaajili ya safari yako, kama kuna cha kuongezea basi wengine watakuja kuongezea.
Elli apk Mshana Jr Depal Paula Paul RRONDO