Kinoo ndiyo nini hiko na kibwengo mlikitoa wapi🤔Mi niliwahi kuona Jamaa akimkaba kibwengo ili amuibie kinoo chake. Mganga ndiye aliyempa deal huyo mshikaji kuwa kinatakiwa kinoo chá kibwengo. Mimi nilikuwa msindikizaji
Nalog off
Kama nawaona jinsi mlivyokua mnapepeaMakaburi ya Mwananyamala Kwa Kopa kipindi hicho Mama Eliza (R.I.P) ndiye alikua muuza chakula eneo hilo ambalo lilikua linapakana na kituo cha polisi kwa kopa kulikua kuna jini linaranda randa pale.
Fununu zikasambaa sambaa lakini kama ujuavyo kuna siye matomaso.
Kuna jamaa, mmoja wa wapisha wa Mama Eliza, alikutwa kazimia. Alivyozinduka akasema alikumbana na hilo jini.
Matomaso tukapinga.
Kipindi kile yale makaburi yalikua yamezungushiwa seng'enge na ule uwanja wa pembeni ilikua ndiyo tunautumia kucheza mpira, tukimaliza kucheza tutakaa mpaka giza kidogo kisha tunatawanyika.
Siku hiyo tukawa tumekaa pembeni ya banda la Mama Eliza tukiwa pale tunauona upande wa makaburini kwa uwazi kabisa.
Giza likiwa linaelekea kushika hatamu tukaona kuna mwanamke anatokea makaburini anakuja usawa wetu. Sisi tukaendelea na stori halafu ikawa kama vile wote tumeambiana kwamba tumuangalie vizuri so wote tukaelekeza macho kule.
Yule mwanamke ni mrefu kawaida tu, amevaa gauni rangi yake ni cream anatembea taratibu lakini kuna kitu wote tukagundua, alikua hatembei kwa kuruka, yaani si unajua ukipita makaburini kuna ile unaruka kaburi hili au lile so unakua hauna muondoko wa aina moja.
But that lady alikua anatembea with easy katika makaburi yaliyorundikana kiasi kile. Almost naweza sema alikua anaelea.
Tukazidi kukaza macho uelekeo wake.
Kisha akafika kwenye usawa wa seng'enge, matarajio ni ainame apite katikati ya seng'enge.
Wrong.
Alipita vile vile akiwa amesimama, hamna kuinama,hamna kukwamishwa na seng'enge. Alipita wima wima na muondoko ule ule wa taratibu.
Baada ya hilo tukio hakuna aliyebaki tulitoka mbio tukaenda kusimama Big M.
Kwavile nalipwa au siyo?Mkuu unajua kutunga..😂
Kipaji tu..Kwavile nalipwa au siyo?
Duh, hayo ni maajabu sana..mfano mngekuwa na ujasiri mngewashtua wale watu sijui ingekuajeNakumbuka ilikuwa mwaka 2005,kipindi hiko Nina miaka km 12,tulikuwa tumelala mapema sn ile siku.Mdogo wangu aliyenifuata baada ya mm kuzaliwa akaniamsha nimsindize chooni,nikaamka nikampeleka.Tulipofika sebuleni nikaangalia saa ukutani ilikuwa km saa 7 usiku,nikafungua mlango wa uani nikampeleka dogo toilet.choo kilikuwa mbali kidogo na nyumba ilipo
Wakati dogo ameshaingia chooni nami nipo nje namsubiria,ghafla! nikasikia Ngoma kama dufu la waislamu zinapigwa na watu zaidi ya ishirini wanaimba..Ilikuwa wanaimba lugha nisiyoielewa huku wanakuja barabarani karibia na usawa wa pale chooni,nakumbuka wale watu Walikuwa wanaume watupu waliovalia nguo nyeupe sn km kanzu.Nikakimbilia chooni,tukawa tunawachungulia jinsi wanavyoimba na kucheza huku wanatembea taratibu Hadi wakatokomea machoni
Waliposepa tukakimbia ndani na kufungua mlango Kwa nguvu sn Hadi wazazi wakaamka.Wakauliza nn tatizo mbn mna hofu hivi ,tukawajibu tulienda chooni lkn tumekutana na watu wasiojulikana wanacheza Ngoma na kuimba.Fadha akafungua mlango akatoka nje akaangalia hajaona chochote akasema itakuwa ni wenge Tu nendeni mkalale
Cha ajabu asubuhi tulipoamka pale nje kwenye Ile njia waliyopita wale watu usiku tukazikuta Ngoma nne zile za mviringo za kupigia dufu na Ngoma moja inalia vigololi ndani.Zile Ngoma zilikuwa mpya kabisa ambazo km hazikuwahi kutumika.Watu wa pale mtaani wakawa wanashangaa zimetokea wapi lkn wazee wakakumbuka usiku tulivyowasimulia lkn hawakuamini now ndy wanaamini.Nakumbuka fadha alifanya utafiti kuhusu wale jamaa huko tuliposema wamekwenda km kuna mtu aliwaona,lkn hakuna mtu yeyote aliyewasikia wala kuwaona huo usiku
Wazee waliohofu pengine tungepata madhara Kwa tuliyoyaona usiku ule lkn hatukupatwa na chochote na Hadi Leo hii hakuna aliyejua wale Walikuwa akina Nani na Kwa nn waliacha Ngoma pale nje
Ni maajabu makubwa na imebaki kuwa fumbo Hadi leo.. samtaimz namuulizaga dogo;hivi unadhani wale jamaa wanaweza kuwa akina Nani naye Hadi Leo Hana jibu na wala pale mtaani hakukuwa na tetesi zozote kuhusu hao watu hadi hv sasa..Nadhani km zisingeonekana zile Ngoma Ile asubuhi watu wasingeamini tulichokiona usikuDuh,hayo ni maajabu sana..mfano mngekuwa na ujasiri mngewashtua wale watu sijui ingekuaje