Kuna siku
Mafian cartel aliuliza kuhusu viungo vya kuweka kwenye nyama ili iwe tamu.
Chukua tangawizi uliyoandaa mwenyewe,
Saga vitunguu saumu,
Weka na vinegar.
Osha nyama vizuri then uweke viungo.
Changanya na chumvi
Itunze kwenye jokofu,usipike muda huohuo
Ukiipika kuanzia kesho yake,viungo vinakuwa vimeenea vizuri .. inakuwa tamu sana..
Mimi huwa natunza ya kupika hata wiki 2
Maana nabadilisha mboga,si kila siku ntakula nyama.
Pia wakati wa kupika,uwe unaweka maji taratibu..yakipungua unaongeza kidogo kidogo hadi nyama iive.
Kama uliweka viungo hivyo,nyama inaiva haraka..pia huwa nakata vipande vidogo vidogo sana.
Km ni mchemsho basi utaacha maji,,
Km unataka ya kukaanga,
Maji yakikauka weka mafuta,koroga,weka moto mdogo
Add vitunguu,hoho Carrots na viungo vingine unavyopenda..mm natumia carrots kitunguu na hoho tu.
Nyama inakuwa tamu sana.