Ashukuriwe Maulana....!!
Baraka hizi ziwafikie na wengine tele na tele kwa kujaa na kusukwasukwa aka lumbesa.
Namna mlo ulikuwa mtamu kabla hata sijaanza kula ulifanya niufotoe kwenye engo tofautitofauti.....
Hapa, mkono wa bibi ulinitembelea.... pishi limeweza, ladhaaa...!!
Tuache masihara, bibi zangu wote upande wa baba na mama walikuwa wanajua kupika balaa. Yaani ule upishi waswahili wanasema ana mkono wa pishi...
Akishika jungu lolote hata kama umeshiba ukionja tuu utakula maana ladha ya chakula haielezeki...
Huo mkono aliupata mama yangu, kwangu umeteremka kiasi cha mboga...
Nina siku na siku....
Kuna siku nilipika pilau tuu la kawaida tuu na nyama, akaja binamu yangu akala....
Aahahaha hadi akanitongoza kwenye simu, nikamwambia kama huna ujasiri wa kunitongoza uso kwa uso nenda huko mi sio mpemba wa kutongozwa na ndugu.
Ila wanaumeee...!!! Amenikumbusha binamu aliyenifata Sauzi....!!π
NB: Usitilie maanani akili za Kasinde, saa ingine ni alosto ya bangee..π.
Alamsiki.