ninaposema kundi namaanisha ni mkusanyiko wa watu of the same interest the same as Genge. Kundi sometimes refer as Genge.
Najua hizi movement kabla walizianza Kikosi Cha Mizinga, ila walishinda.
Sijaelewa unaposema kikosi walishinda.nadhani ni typing error
kuhusu lile swali lako cloudsfm,mbona hawa jamaa wanawalaumu wao tu!wakati kuna radio station kibao..ni hivi,hii redio na kampun yote kwa ujumla ina nguvu sana kwa sasa ilo hakuna anayeweza kubisha,sasa wanachofanya ni ku-control hii sanaa kwenye kila angle. Wanaushawishi mkubwa na wanautumia uo ushawishi kunyonya na kuibia wasanii na kazi za sanaa..wanachofanya ni kuwajengea UOGA wasanii na wadau wengine wa sanaa wasithubutu kudai haki zao au kuingilia dili mbalimbali za pesa zinazohusu sanaa,uku wakijitamba wao ndio wanasaidia wasanii..ivo hawa ndio mapapa wa wizi wa sanaa ivyo ukiweza kuwadhibiti hawa ata vidagaa vingine inakuwa raisi kudili navyo..
Ngoja nikupe mfano,kuna siku moja kitambo cha nyuma kidogo ata Sugu ajawa mbunge,kulikuwa na lile sekeseke la ishu ya malaria kati ya Ruge na Sugu,baada ya uyu Ruge kutumia sana redio yao kupotosha ukweri,kina Sugu wakaomba kupewa nafasi east africa radio waujulishe umma kinachoendelea,akakubaliwa kufanya interview yeye na wenzake..kilichofuata Sugu,Mkoloni,Gsolo,Mapacha,Dan msimamo na wengine wakafika studio,ilikuwa ijumaa usiku,kipindi cha friday night live,muda mchache kabla ya interview kuanza ikapigwa simu kwa dada mmoja pale ea radio nadhan ni mkubwa wa vipindi,sikumbuki vizuri(simu ilitoka kwa ruge na wanamtandao wake kina january)..yule dada ghafla akawafuata na kuwaambia hawataweza kufanya mahojiano siku ile,ila kama wanataka kuzungumza wasigusie kabisa ishu ya malaria na zinazofanana na izo..nafikiri unaanza kupata picha jinsi gani hawa jamaa wana nguvu na walivyopenya kila kona...alafu unataka wasitukanwe!!??