Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Juzuu hii ina makala moto na ngumu zinazohusu mambo makubwa yaliyowahi kufanyika nchini na ambayo hakuna Mwandishi yeyote aliyewahi kuthubutu kuyasimulia.
Ni shuhuda za mwandishi wa habari mahiri katika bara la Afrika anayeheshimika duniani pote akisimulia mambo makubwa yaliyofanyika katika awamu zote tangu Uhuru wa Nchi hii na pengine hayajawahi kusimuliwa na mwandishi yeyote, yakiwemo vuguvugu la Katiba Mpya la mwaka 2011 na kuundwa kwa G55.
Je, ni wakina nani waliounda kundi hilo?
Je, ni kweli hilo kundi lilikuwa na watu 55?
Kitabu hicho kimesheheni hazina ya taarifa za uchunguzi zinazohusu mambo makubwa ya siasa za Tanzania yakisimuliwa na kuandikwa na mwanaharakati wa miongo minne asiyeyumba wala kuyumbishwa, Jenerali Twaha Ulimwengu!
Pata nakala ya Juzuu la “Rai ya Jenerali” uwajue mashujaa waliosimama kidete kutaka Katiba Mpya na hatma yao.
Juzuu hilo lenye kurasa 234 na makala 37 tayari liko Mtaani kwa bei ya Tsh. 30,000/- tu. Zinatolewa nafasi kwa vijana wenye mtaji wa vitabu kuanzia vitano wanaotaka kujiajiri mahali popote Tanzania kuwasiliana na wasambazaji.
Kuhusu Uzinduzi
Uzinduzi wa Juzuu la “Rai ya Jenerali” utafanyika Agosti 6, 2021. Mgeni Rasmi ni Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa Katiba Mpya 2011, Waziri Mkuu Wa Tanzania 1985 -1990 na Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki.
Juzuu au kitabu kimewekewa sahihi za heshima na Profesa Mark Mwandosya, Dkt. Martha Qorro, Dkt. Azaveli Lwaitama na wengineo.