Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
C&P from Face Book.
THE RIGHT THING AT THE WRONG PEOPLE, IDIOT!
Na Bollen Ngetti
0748 092092
KUNRADHI kwa kuteua kichwa cha andiko hili kuwa katika lugha ya kikoloni. Shabaha ni namna tu ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Naam! Nilikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa kitabu kinachohusu maisha ya Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Sokoine yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam huku mzinduzi akiwa ni Mgombea Urais kupitia CCM 2025 Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika hotuba yake ambayo haikuvutia sana adhira, Rais Samia alichombeza neno akirejea maisha ya Hayati Sokoine na kusema, "ukiwa mwadilifu vyeo vitakufuata huko huko uliko wala huna haja ya kupigania!! Tafakari kibwege!
Ukweli usiopepesa macho ni kwamba Sokoine alikuwa ni mwaminifu na mwadilifu kwa kiwango cha kuudhi. Kwamba kwake kipaumbele kwake ilikuwa ni nchi yake na si familia yake, si marafiki zake, si ndugu zake wala si maswahiba wake. Kwake baada ya Mungu alimsujudu Tanzania. Kiukweli haya ni maisha matukufu ambayo kama viongozi wetu wakiamua kwa dhati kuyaishi nchi hii itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo kuliko haya maendeleo ya mwendo wa kono-kono.
Yapo mambo kadhaa tunapaswa kutafakari kama taifa lenye uhai na uhuru wa miaka zaidi ya 60. Mosi: ule uzinduzi uliandaliwa kina nani? Yani ujumbe wa maisha ya Hayati Sokoine ulikusudiwa kumfikia nani? Macho yangu yaliporambaza ukumbi wa JNICC ukiacha walinzi wa Rais wanaoonekana na wasioonekana japo wanajulikana, waliobaki walikuwa ni wazee (Gen A&B) walioishi na kufanya kazi na Hayati Sokoine wakiongozwa na kina Joseph Warioba, Steven Wasira, Joseph Butiku nakadhalika.
Yani nimeishi na baba yangu tangu utotoni hadi uzeeni halafu mtu mwingine aje kunielekeza na kuniadithia maisha ya Mzee Ngetti. Kweli? Kwamba pale kina Wasira wafundishwe maisha ya Sokoine? Kwamba wamsome Sokoine? Jinga kabisa! Hivi ni mzee gani alitoka pale amenunua kitabu? Hakuna hata mmoja.
Hilo la kwanza. Kwamba nilitegemea waalikwa wakuu katika uzinduzi ule wangekuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati na hata wa Sekondari kwa maana ya Gen Z ambao hawajui kabisa kabisa maisha na uongozi wa Sokoine. Kwao hayo maisha ya Gen A&B ni upuuzi mtupu maana maisha ya viongozi wa sasa yanawalazisha kuwaza wizi, ufisadi na rushwa.
Wanajiuliza kama kweli ukiwa mwadilifu ni kweli vyeo vinakufuata? Wanawatazama baadhi ya watoto wa viongozi kama Ridhiwan, January Makamba, Mohamed Mchengerwa, Godfrey Pinda, Hussein Mwinyi, kutaja kwa uchache. Je, uadilifu wao ndio vyeo vimewafuata au ni marina ya baba zao na patronage politics (vimemo na viunganishi).
Kwa mwenendo huo walengwa ambao hawakualikwa watajifunza wapi na kwa namna gani maisha ya Sokoine? Kwani Nape si alituambia namna ya kushinda uchaguzi na kuongoza watu? Kwamba usitegemee vyeo kukufuata bali ni wewe kuvifuata kwa kujambazi kura? Tunao waadilifu kibao wanaozea mitaani maana hawana viunganishi kama kina Abdul Suluhu Hassan.
Nihitimishe kwa kusema uzinduzi huu haukuwafikia walengwa ambao ni Gen Z. Lakini pia ujumbe wa Samia kuhusu uadilifu haukidhi vigezo vinavyoshuhudiwa kwa sasa. Hakuna Gen Z yuko tayari kiyaishi maisha ya Sokoine maana kwanza wanabaguliwa katika uhalisia ila majukwaani wanarembwa na kuambiwa wagombee nafasi za uongozi.
Mwisho ni jambo jema kuwa na maandiko na machapisho kuhusu maisha ya kiuongozi juu ya maisha ya viongozi wetu. With wa familia ya Sokoine kwamba Serikali isaidie kusapoti maandiko juu ya maisha yao maana kweli wengi wanatamani kuandika lakini wamechoka, hawana fedha hivyo watapotea hivi hivi.
Nina ushahidi ninao. Niliwahi kuomba msaada Ikulu kuandika kitabu kihusucho maisha ya Samia Suluhu Hassan kabla ya kuwa Rais, Uongozi wake na Visheni yake. Nilipigiwa simu na Ikulu na kuambiwa, "wewe kama unaandika kitabu hicho endelea tu kama wewe. Hakuna fedha hiyo kutoka Ikulu". Nilikata tamaa!
Hii ndio maana nasema kilichofanyika ni "Right Thing to The Wrong People "! Idiot.