Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara

Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Leo Julai 26, 2019 Mhe. Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye uwekaji jiwe la msingi la mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji

Rais Magufuli aliwasili Rufiji akitokea Dar es Salaam akitumia treni ya reli ya TAZARA kwa kupitia Fuga na Kisaki



UPDATE:
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani;


Rais ulipotuita Ikulu kutueleza ndoto yako kuhusu mradi huu, wengi hatukuelewa lakini sasa tumeanza kukuelewa. Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 42 na mpaka sasa umeshatekelezwa kwa miezi 6

Dkt. Kalemani: Mradi huu utakapokamilika utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitatumika kuendesha treni ya umeme. Umeme huu pia utasafirishwa hadi Chalinze na baadaye Dar es Salaam na Dodoma. Tunatazamia utasaidia sana kuendesha viwanda hapo baadaye

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kampuni hizi zinazojenga mradi huu zimefanya maajabu makubwa kule nchini Misri. Pacha wako Rais wa Misri, Fattah al-Sisi amejenga Mfereji wa Suez mwingine ndani ya kipindi kifupi. Nyie Marais nyieeee

Rais Magufuli:
Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo‬. Napenda kumshukuru Waziri wa Nishati kwa kunialika, nawashukuru pia Mabalozi na wageni wetu kutoka Misri. Hiki ni kielelezo cha urafiki‬

Hapa kwetu umeme unauzwa zaidi ya senti 11, gharama za umeme zinafanya kupanda kwa bei ya bidhaa na mwisho haziwezi kushindana kwenye soko. Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni Taifa huru, mradi huu umepata upinzani kutoka nje na ndani

Nchi yetu ni huru na wala sio masikini, tuliamua kujenga kwa fedha zetu za ndani kupitia kodi zinazokusanywa kutoka kwa Wananchi. Fedha hizi watalipwa Waafrika wenzetu, hii ni ishara kuwa Waafrika tukiamua tunaweza

Huku kuna sehemu chumba kimoja mtu analala kwa dola 3,000. Watu wanakuja na kuondoka huku. Sijui kama Mawaziri mnajua hizo fedha tunapata asilimia ngapi, wala sijui kama vyombo vya usalama vinajua mali kiasi gani inasafirishwa kutoka hapa

Kiasi cha umeme kitakachozalishwa hapa hakijawahi kuzalishwa katika historia ya nchi yetu. Kwa sasa nchi yetu inazalisha umeme Megawati 1,601. Natarajia umeme utakaozalishwa hapa utasaidia kushusha gharama za umeme

Tanzania inaongoza kwa utunzaji wa mazingira. Maeneo tuliyoyatenga ni makubwa mno. Mradi huu utaongeza fursa katika sekta ya kilimo. Kule Mtera na Nyumba ya Mungu shughuli za uvuvi zilishamiri baada ya ujenzi wa mabwawa

Kwenye hii Selous kuna maeneo ya kuwindia (Hunting Block) 47 watu wanakuwa wanaua Simba wanaondoka na gharama kwa mwezi ni Dola 5,000. Ukilipa hiyo unaruhusiwa kuwinda hata ukiua Nyati 10. Ukweli uwindaji haulipi kwenye hii mbuga

Naomba kuanzia leo hili eneo la uwindaji likatwe, tulifanye kuwa National Park. Mataifa mengine hayafanyi sana hizi shughuli. Waziri uende ukakae kwenye Wizara mkapunguze eneo la uwindaji, hilo limesemwa sana lakini utekelezaji umechelewa

Hapa kuna 'Hunting Block' za uwindaji sijasema zifutwe. Na kwa sababu ziko eneo la chini basi eneo la juu ligeuzwe kuwa National Park na iitwe Nyerere National Park. Bwawa liitwe Bwawa la Nyerere ili vizazi vijavyo vikumbuke mambo mazuri ya Nyerere

Juzi zimerudishwa Dhahabu kutoka Kenya ambazo thamani yake ni zaidi ya bilioni 5, hizo Fedha zianze kujenga barabara kutoka Fuga kuja hapa. Tuanze kutengeneza pole pole hizi Kilomita 60. Leo watu wanaweza wasielewe

Serikali imeendelea kutekeleza miradi mingine na tunatekeleza miradi mikubwa ya kusafirisha umeme. Naipongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa miradi hii ambayo imepunguza mgao wa umeme. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

Kutokana na TANESCO kupunguza kuagiza vifaa kama nguzo na 'transformer' kutoka nje, Viwanda 15 vimeanzishwa na kuzalisha ajira zaidi ya 3,000. Niwasisitize Wakandarasi kutekeleza mradi huu ndani ya wakati na unatarajiwa kutimia Juni 2022

Kumekuwa na mabishano kati ya NIC(Wanaotoa Bima), TANESCO na Makampuni yanayojenga hapa. Bima lazima itolewe na Serikali, ole wenu akasaini Bima na mtu mwingine. Vibali vya Wafanyakazi vitolewe mapema lakini isiwe utolewaji holela

Wananchi wa eneo hili ndio wakapewe kipaumbele cha ajira kwa sababu wao ndio wamelilinda pori hili tangu kuumbwa kwa dunia. Vyombo vya ulinzi na usalama, viuchukue mradi huu kama mboni ya nchi. Nitashangaa kama JKT hawatahusika kufanya kazi hapa

Natoa wito kwa Wizara kuanza kutekeleza kuzalisha umeme kwa njia nyingine kama jua, joto na upepo. Wananchi kama Pwagu wa kule Njombe wanaojitokeza kuzalisha umeme waungwe mkono kwani wanaweza kuzalisha umeme katika vijiji vyao

Ndugu zangu Wananchi namalizia na maneno haya, 'Ukiona umeenda kwenye pori na nyuki ni wakali sana ujue kuna asali'. Hapa kuna asali ndio maana watu walipiga kelele. Ukiamua kufanya mradi wako fanya usisubiri watu wakushauri

Huku kuna hoteli kubwa kuliko hoteli za Dar es Salaam. Chumba kimoja dola 3,000 na ina vyumba 15. Sijui kama Serikali inapata mapato. Muda wa kuchangamka ni sasa. Wizara ya Maliasili kagueni hiyo hoteli mjue Serikali inaingiza kiasi gani.

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA


HISTORIA

 
Endelea kutuhabarisha mkuu. Naiona Tanzania mpya ya kesho inavyojengwa na Rais Mzalendo, JPM
Mkuu ukipigiwa simu ukaona jina la nape, zima simu yako haraka sana, utoe betri halafu uiweke kwenye sanduku la chuma, halafu hilo sanduku ulifiche uvunguni, uondoke nyumbani haraka sana uende huko stieglers gorge ukakae mwezi mzima ndiyo urudi nyumbani usije ukaingia kwenye matatizo kabla Cheusi Mangala hajarusha clip yako hadharani.
 
Hongera sana Mhe Rais JPM wewe ni Rais utakaetuvusha pale tulipokuwa....hata waseme nini ila kimoyomoyo wanakubali utendaji wako uliotukuka kabisa.....nakupenda sana Mh Raisi sijutiii kura yangu ya 2015 katikati ya masokwe watu waliokuwa wakizungusha mikono
 
Nilijua tu mambo ya live jamaa ni mzima sana na kila mtu anaweza kubahatisha ataongelea nini.

Mie nasubiri kwa hamu agusie kuhusu clips za wapumbavu wa mwaka.
 
Endelea kutuhabarisha mkuu. Naiona Tanzania mpya ya kesho inavyojengwa na Rais Mzalendo, JPM
Kaka sijui dada maana hizi Id fake hizi hazina jinsia.

Ila ukweli ni kwamba, jiwe akitoka madarakani ndo utakiona Tz mpya kwa sasa tunaaminishwa tu, uhalisia wake binafsi sijaona. Ninacho kuona ni uoga wa kuchoma madaraka baada ya, damu walizomwaga ingawa ni kwa siri, upendeleo, undugu, kutofaata sheria na kuwaingiza wananchi kwenye maisha magumu zaidi.

Haya utayaona akikubali kuondoka baada ya mda wake, ila hilo ninawasiwasi nalo kwa mwendo huu.
 
Back
Top Bottom