Chama cha Mapinduzi (CCM) kinafanya mkutano wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani Temeke. Mkutano huo umeanza rasmi maandalizi kuelekea uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 27 Novemba.
View: https://www.youtube.com/live/Acl2q9uw3O8
=====
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amesema;
"Leo ni hatua nyingine baada ya hatua mbalimbali kupita. "Nataka niwakumbushe kwamba mpaka tunafika hapa siku ya leo ya kuanza kampeni nchini nzima, tumepitia mchakato wa matukio mbalimbali. Vyama vya siasa vilipewa fursa kupitia 4R za Rais Dkt. Samia kuruhusu mikutano ya siasa ifanyike, maana yake tulianza na mchakato wa kwanza wa kuandaa wananchi wetu kuhusu uchaguzi (maandalizi ya umma). Chama cha Mapinduzi kilifanya kazi hiyo vizuri kabisa, kuanzia viongozi wa kitaifa mpaka viongozi wa mashina ambao wamefanya kazi nzuri kwa chama cha Mapinduzi."
"Umma wa Tanzania ulielewa kwamba mwaka huu kutakuwa na uchaguzi na umuhimu wa uchaguzi huo. Nyie ni mashahidi viongozi. Sekretarieti ya Chama ikiongozwa na Katibu Mkuu tumezunguka mikoa 20 kuandaa umma wa Watanzania. Jumuiya za chama zimefanya kazi hiyo kubwa kuandaa umma wa Watanzania. Kwahiyo, mchakato huo chama cha Mapinduzi kilifanya kazi kubwa na ndio maana Watanzania wengi wakaelewa kwamba mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi."
"Sitaki kuwasemea wengine, lakini wakati tunafanya kazi hizo, nao walifanya kazi zao. Mlisikia maandamano, hamkusikia habari ya uchaguzi, mlisikia habari ya katiba mpya, lakini viongozi wa CCM na jumuiya zake zilijikita kutatua kero za wananchi, kueleza utekelezaji wa ilani na kuandaa Watanzania juu ya uchaguzi."
"Katika chaguzi zote zilizopita, uchaguzi wa safari hii hamasa ya kujiandikisha ilikuwa kubwa sana. Dar es Salaam inatajwa kuwa mkoa uliofanya vizuri katika uandikishaji, ambapo zaidi ya watu milioni 3 wameandikishwa. Sitaki kuwasemea wengine, nilisikia wanalalamikia wanasema uandikishaji wananchi hawajahamasishwa. Niliwauliza, wakati tunafanya ile kazi, nyie mlikuwa wapi? Unataka uhamasishwe na watu?"