Uzinduzi wa kanisa la Mwamposa na maswali ya kujiuliza

Mwamposa ni mradi wa kisiasa kuelekea uchaguzi Mkuu, plus wale wapambe wenzake wakina Maboya.
 
ndugu zangu, kitu cha kweli ambacho kuna siku mtakuja kutoa ushuhuda hapa ni kwamba, mchungaji yeyote, mtume yeyote ambaye anafanana manyoya na serikali ya ccm, huyo sio wa Mungu. nakuhakikishieni hili, na hata wale wa jana wote ukiwaangalia, walijaa wale wahuni wahuni wa injili ambao wanahitaji ulinzi wa serikali, wanahitaji kuwa upande wa serikali kwa sababu kutokana na wayayoyafanya wakiwa kinyume na serikali hawatasavaivu. tumaini lao ni Rais wa nchi, ni mawaziri, ni mapolisi. ila kuna watu wamenyimwa haki ya kuabudu hao tumaini lao ni Mungu mwenyewe, hawana pa kusemea ila kwa Mungu, hawana mapolisi ila Mungu, hawana rais ila Mungu, hawana bashungwa ila Mungu, Mungu ndiye kimbilio lao. hao wanaotegemea wanadamu ipo siku hao wanadamu wakiondoshwa na Mungu tumaini lao litakuwa wapi?

YEREMIA 17:5; BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mwamposa, maboya, na wachungaji woote walioleta kebehi jana, tumaini lenu ni Rais wa nchi, mawaziri na mapolisi, na mmesifiwa na kutukuzwa sana, mmekwisha pata thawabu yenu, mtakula matunda ya hao mnaoungana nao kusimanga wale wanaonyimwa haki ya kuabudu. Mungu atajitwalia utukufu peke yake bila msaada wa polisi, Rais, mawaziri au wakuu wa mikoa. mark my words.
 
"Vijana wanamiminika kuombewa wapate ajira katikati ya eneo lillokuwa linazalisha ajira"🎯
 
Kilikuwa kiwanda bora Tanganika na EAC nzima. Bidhaa zake ziliuzwa nchi za nje na humu ndani ya nchi maduka makubwa kama Oysterbay Super Market haya kukosa kusheheni nyama za kopo zilizosindikwa Tanganyika Packers......
Kwa SASA ni awamu ya kusindika misukule na mafisadi kwenye hema la Mwaposa..... Ama kweli wajinga ndio waliwao.😎
 
Kwa hiyo unaiongelea Tanzania packers ka vile Mwamposa ndiye aloiyesababisha kiwanda hicho kife,je na viwanda vingine lukuki vilivyokufa mfano Mwatex,Urafiki,Ufi,ZZK,n.k navyo mbona huviongelei? au sababu Mwamposa hayupo kwenye viwanja vyake? Halafu umeandika waumini wa Mwamposa wananyweshwa udongo,hakuna mtu amewahi nyweshwa udongo na Mwamposa,wewe ni mpotoshaji wa kawaida sana,uandishi wako ni uandishi ambao upo biased na upingaji wa ukristo.
 
Kwa hiyo unaiongelea Tanzania packers ka vile Mwamposa ndiye aloiyesababisha kiwanda hicho kife,je na viwanda vingine lukuki vilivyokufa mfano Mwatex,Urafiki,Ufi,ZZK,n.k navyo mbona huviongelei? au sababu Mwamposa hayupo kwenye viwanja vyake? Halafu umeandika waumini wa Mwamposa wananyweshwa udongo,hakuna mtu amewahi nyweshwa udongo na Mwamposa,wewe ni mpotoshaji wa kawaida sana,uandishi wako ni uandishi ambao upo biased na upingaji wa ukristo
 
Ndugu soma uelewe mwandishi anamaanisha nini, achana na mihemuko!
 
Hata hizo zilizofika ni nyama zilizo be packed Ili Zi tick October!

KAZI na Utu tunasonga mbele!
Mnasonga mbele kwenda wapi au kuongeza deni la taifa liwe trilioni 200 mwakani?

Kazi ipi ?

Huo utu mlimaanisha utumwa mkapunguza herufi za mwisho?
 
Mwamposa, maboya, na wachungaji woote walioleta kebehi jana, tumaini lenu ni Rais wa nchi, mawaziri na mapolisi, na mmesifiwa na kutukuzwa sana, mmekwisha pata thawabu yenu, mtakula matunda ya hao mnaoungana nao kusimanga wale wanaonyimwa haki ya kuabudu. Mungu atajitwalia utukufu peke yake bila msaada wa polisi, Rais, mawaziri au wakuu wa mikoa. mark my words.✌🏿✌🏿✌🏿
 
Huu ni uwendawazimu wa kiwango cha juu sana.

Yaani kutoka kiwanda cha kuzalisha mapato, nyama na ajira! mpaka kuwa jengo la kuwaibia wajinga kwa kuwafanyia miujiza feki na kuwauzia bidhaa za kawaida kama maji, mafuta, udongo, nk. kwa bei ya kulangua kwa kisingizio cha upako wa uongo!!
 
Tanzania ni ya pili Africa kuwa na Ngombe wengi,nadhani nyuma ya Sudan.

Kuna fursa kubwa sana hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…