Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UZINDUZI WA "MWANAMKE MWANAMAPINDUZI" GOLDEN TULIP
Ikiwa ulipitwa na yaliyoelezwa kuhusu kitabu hiki:
Hiki ni kitabu kinachohusu maisha ya Biubwa Amour Zahor kilichoandikwa na Zuhura Yunus.
Kitabu hiki kinahusu maisha yake Biubwa akiwa msichana mdogo wa Kiarabu katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.
Nilipoanza kukisoma kitabu ghafla ikanijia kichwani filamu fupi niliyooana udogoni ya siku ‘’El Comandante,’’ Fidel Castro alipoingia Havana baada ya kumuangusha Fulgencio Batista.
Pamoja na Castro ile filamu ilikuwa ikimuonyesha msichana kavaa unifomu za jeshi amebaba bunduki na kashika, ‘’megaphone,’’ anatoa matangazo akiwa juu kwenye gari lililojaa askari Wapinduzi (neno hili nimejifunza ndani ya kitabu hiki mwalimu wangu mwandishi wa kitabu Zuhura Yunus).
Kweli bint huyu kashuka kutoka Sierra Maestra na Fidel Castro na hakuna shaka ni mwanamke shujaa mpiganaji.
Lakini ushujaa wake haufikii hata robo ujasiri wa Biubwa kwani mwanamke wa Cuba huwezi kumfananisha na mtoto wa kike wa Kiunguja.
Fikra zangu zikashuka kutoka kwa huyu bint zikenda Zanzibar katika hekaheka ya mapinduzi.
Ndani ya kitabu hiki kuna picha ya Biubwa mwanamke pekee kisha wa Kiarabu katikati ya wanaume Wapinduzi ameshika bunduki kama vile kashika kikapu anaelekea Soko Muhogo.
Biubwa mwanachama wa ASP kashiriki katika mapinduzi ya kuiangusha serikali ya mseto wa ZNP na ZPPP.
Mapinduzi yaliyojaa umwagaji wa damu ambayo harufu ya damu ile haijapata kwisha.
Biubwa kafikaje hapa?
Biubwa kujifunza wapi silaha, lini na nani mwalimu wake?
Lakini kitabu hiki cha maisha ya Biubwa Amour Zahor si kitabu utakishika na kukiacha.
Salama yako katika kitabu hiki ni wala usikiguse.
Ukikigusa ni sawa na ndege shorwa katua katika ulimbo.
Ndege huyu mdogo wa umbo akitua kwenye ulimbo huwa hawezi kwamwe kujinasua mwenyewe.
Ukikigusa kitabu hiki ukakifungua na kuanza kusoma basi jua ushanasa.
Hiki si kitabu cha maskhara.
Shaaban Robert alipata kuandika kitabu, ‘’Ashiki Kitabu Hiki.’’
Mimi nakusihi na nakuambia maneno haya, ‘’Kisome kitabu hiki.’’
Kitabu "Mwanamke Mwanamapinduzi," kinachohadithia maisha ya Biubwa Amour Zahor ni, "thriller," katika viwango vya James Bond.
Zuhura Yunus mwandishi wa kitabu hiki kaifanyia hisani kubwa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.
Mwisho wa kitabu Zuhura Yunus anakipasua kichwa chake na katika kufanya hivyo anatupasua hata na sisi wasomaji wake pale anapopitia maisha ya Biubwa toka udogoni katika usichana hadi kufikia sasa ni mwanamke na ana akili zake kamili.
Hapa ni baada ya mapinduzi na Biubwa kampoteza baba yake kwa kuuliwa akiwa kifungoni.
Kifo hiki ni kilele cha hadithi ya kusikitisha katika maisha ya Biubwa.
Zuhura Yunus sasa ni kama vile anatuambia wasomaji wake tukisome kitabu cha maisha ya Biubwa huku tukitafakari kila neno aliloandika katika mstari kupata kile ambacho huenda labda kimejificha.
Kwa hakika ikiwa msomaji hatofanya hivyo atakuwa kajipunja mwenyewe.
Kukifaidi kitabu hiki msomaji lazima aingie na atembee tena kwa utulivu, atembee kwa miguu yake mwenyewe katikati ya kila mstari anaosoma ndani ya kitabu hiki.
Hakuna njia ya pili.
Angalia mkasa huu wa Mzee Karume na Engen.
Okello, Engen na wenzake walikamilisha kazi yao na Mzee Karume akawaahidi kuwapa ujira wao kwa maandishi.
Hapa ndipo Engen alipopokea barua yake kutoka kwa Mzee Karume.
Sijui kwa nini Zuhura Yumus hakuita hii barua kuwa ni mkataba kati ya Karume na Engen.
Barua hii kwa vyovyote vile itakavyokuwa kwa Engen kwanza ilikuwa mfano wa yeye kupewa mgodi wa dhahabu.
Pili barua ile ilikuwa ushahidi tosha kwa yote yaliyopitika Zanzibar kufanikisha mapinduzi Engen akiwa muhusika mkuu.
Lakini kubwa na sijui kama Engen alilitambua ni kuwa barua ile ilikuwa mkataba wa yeye na wenzake mfano wa yeye kuua watu kwa ajili ya fedha.
Akiwa amekikalia kiti barabara Karume hakuwa na nia ya kutimiza ahadi yake si kwa Engen, John Okello au yeyote yule.
Karume aliitaka barua yake irejeshwe kwake kwa njia yeyote ile.
Nani shujaa anaemwamini anaeweza kufanya kazi hii?
Hapa ndipo Waingereza wana msemo.
Msomaji wa kitabu hiki, "will have to burn the midnight oil."
Karume hakumwamini hata Mussa Makungu Mkuu wa Usalama wa Baraza la Mapinduzi wala hakuiamini ile, "Kamati ya Watu 14," ya Seif Bakari.
Karume aliomba msaada wa Biubwa amrejeshee barua yake.
Huu ni mfano wa, "The Tamarind Seed," na lile "Blue File," la Warusi lililotakiwa na Waingereza.
Hapa ndipo Zuhura Yunus mwandishi aliyetuandikia hiki kitabu alipotokwa jasho yeye na kwa "roho yake mbaya," akaona asife peke yake atuchukue na sisi katika safari yake hii ya mwisho.
Zuhura alipokuwa sasa hayuko tena na Biubwa bali yuko peke yake anamtafakari Biubwa Mwanamapinduzi anataka ayajue yale ambayo bila shaka Biubwa hakumweleza.
Biubwa si mwanamke mwananapinduzi wa kawaida.
Wanafunzi wa historia ya Zanzibar wamepewa zawadi kubwa katika kitabu hiki.