Uzinduzi wa Leseni Kwa wahandisi waliosajiriwa

Uzinduzi wa Leseni Kwa wahandisi waliosajiriwa

Tangawizi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Posts
6,696
Reaction score
6,734
Leo, Dr. Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi amezindua rasmi matumizi ya leseni kwa ajiri ya practising engineers and engineering consultants kama sheria inavyoelekeza.
Moja ya mambo muhimu aliyoyagusia ni bodi ya wahandisi sasa kuwa mstari wa mbele kutoa ushauri mbadala kwa serikali katika mambo muhimu yanayohusu uhandisi, bila kusubiri kutumwa au kusukumwa kama ilivyo sasa.
Kwa mtazamo wangu, Magufuli amesema kitu muhimu sana maana imekuwa kama ni tabia sasa wahandisi kuacha fani na kuwa wanasiasa hata kwa kazi zilizo za kitaalamu.
Bila ushiriki wa dhati wa wahandisi katika kuhakikisha ubora wa kazi zinazofanywa na kupiga vita rushwa, nchi hii haitakaa kuja kujengeka. Ni aibu kuona wahandisi wanachangia kwa kiasi kikubwa kuchakachua ubora wa kazi zinazofanywa....naamini Dr. Magufuli ametoa changamoto....kazi kwa wahandisi sasa kuona nasi tunacheza sehemu yetu....tukumbuke, heshima yetu itajengwa na matendo yetu na siyo vinginevyo!! Tuache kupiga domo na kuwa waadilifu tukifanya kazi.
 
Sidhani kama itapunguza kasi ya professionals kwenda kwenye siasa, tatizo kuu malipo, ineonekana siasa inalipa kuliko professions.
 
Back
Top Bottom