TAARIFA KWA WANACHAMA, WANANCHI NA WAPENZI WA CHADEMA TANZANIA
Ndugu wanachama, Wananchi na wapenzi wa CHADEMA,
Tunapenda kuwajulisha kuwa tarehe ya uzinduzi wa Operation #NoReforms, NoElection – Kanda ya Nyasa (Mbeya) imebadilishwa kutoka 23 Machi 2025 hadi 1 Aprili 2025.
Marekebisho haya yamefanywa kutokana na sababu za kifedha na maandalizi yanayohitaji muda wa ziada ili kuhakikisha uzinduzi unafanyika kwa mafanikio makubwa na kwa ufanisi wa hali ya juu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na tunawashukuru kwa uvumilivu wenu. Tunaendelea kuwasihi muendelee kuwa na hamasa, mshikamano, na utayari kwa siku hiyo muhimu.
Kamati ya Maandalizi:
Operation No Reforms, NoElection
Kanda ya Nyasa - Mbeya.

- Tunachokijua
- 'No Reforms No Election' ni ajenda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA yenye lengo la kuhamasisha mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi. Ajenda hiyo imekuwa na mapendekezo mbalimbali yanayopaswa kufanyika ili kuwe na uchaguzi huru na wazi ambapo inasisitiza pasipo na mabadiliko hayo hakuna uchaguzi.
Machi 19, 2024 Naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Amani Golugwa alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo pamoja mambo mengine alitangaza kuwa, kuanzia tarehe 23 Machi 2025 viongozi wakuu wa Chama hicho wataanza ziara ya mikutano ya hadhara nchi nzima, huku mikutano hiyo ikitarajiwa kuanza katika Kanda ya Nyasa na mkutano wa kwanza kufanyika katika jiji la Mbeya huku ikibainishwa kuwa sehemu ya uzinduzi wa Oparesheni ya 'No Reforms No Election'
Madai
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa tarehe ya uzinduzi wa Oparesheni ya No Reforms, No Election Kanda ya Nyasa uliotarajiwa kufanyika jijini Mbeya imebadilishwa kutoka 23 Machi 2025 hadi 1 Aprili 2025.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ukihusisha utafutaji wa kimtandao kwa kutumia maneno muhimu (Key word search) umebaini kuwa taarifa hiyo haijatolewa ama kuchapishwa na CHADEMA kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Aidha chapisho linaloonesha mabadiliko ya tarehe ya uzinduzi huo limepotoshwa kwani limehaririwa kwa kubadilishiwa tarehe kutoka kwenye chapisho la awali lililokuwa na Picha ya Tundu Lissu likiwa na tarehe 23, Machi 2025 tofauti na lililopotoshwa.
Hata hivyo CHADEMA wameendelea kufanya uhamasishaji kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuelekea uzinduzi wa ajenda ya No Reforms No Election huku tarehe ikisalia kuwa Machi 23, 2025. Rejea hapa na hapa.
Pia, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Masaga Kaloli ameiambia JamiiCheck kuwa “Si taarifa za kweli, kila kitu kipo palepale kulingana na ratiba yetu na mchakato unafanyika leo (Machi 23, 2025), wanaosambaza hizo taarifa wana nia potofu.”