Uzinzi haulipi

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,153
Reaction score
809
Wakuu leo naingia kwenye jukwaa hili kuwashauri wana MMU wenzangu, tuache uzinzi.

Uzinzi haulipi, ebu jiulize kwa nini uishi kwa wasiwasi kila siku, wasiwasi wa kuwa na UKIMWI. Wasiwasi wa kuacha familia yako shauri ya UKIMWI, wasiwasi wa kwenda kupima mke wako anapopapata ujauzito. Wasiwasi pale unapoangalia watoto wako ukiwa na mawazo kuwa wewe ni baba/ mama mwathirika,kuwa mwaminifu. wanawake hupenda kulipa kisasi. wanawake hupenda kufata tabia za waume wao, kuwa big dady siyo dady UKIMWI tu.

Kwa Mkristo mwenzangu, uwe waaminifu katika maisha ya ukristo wako. nenda kusali. Anzisha kanisa la kiroho nyumbani. Sara za jioni za asubuhi. Soma neno la Mungu funga na kuomba. Umeshamchagua mwenza wako. Komaa acha kifo kiwatenganishe. Tunza watoto wako na jamii yako. Biblia inasema wazinzi kwao ni kwenye ziwa la moto.

Na kama Muislamu, Uwe na hofu ya Mungu kazana kuswali, funga kuwa busy. Uislamu hauruhusu uzinzi sawasawa na kwa Ukriksto ambapo uzinzi ni marufuku. Pia kama unatamani uoe.Chagua wazuri wazuri mpaka wafikie wanne.
Kataa kuishi maisha ya wasiwasi kataa kuisha maisha ya kuogopa kataa kuishi na ya kufikiria UKIMWI komaa na mke/ mume wako. Si ulimchangua mwenyewe.

Chondechonde ndugu zangu wanaume kwa wanawake tubaki njia kuu mchepuko sio dili.
Kwa wote wanaopenda familia zao wataniunga mkono.
 
Njia kuu wanaenda wengi,njia nyembamba wanaenda wachache maana ndo inaenda uzimani.
 
Ndo umeandika nini, au yamekukuta tayari
 
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi, majivuno na njia mbovu, Na kinywa cha ukahidi pia nakichukia. Mithali 8:13
 
Ndo umeandika nini, au yamekukuta tayari
Kweli mkuu, nimesoma sijamuelewa kabisa. Tujitahidi kujenga Hoja zenye mashiko tofauti na kupayuka. Mpe mtu sbb ya kuacha kufanya jambo fulani badala ya kumkataza.
 
Ulianza vizuri sana.. Ila umeharisha vibaya unaposema ukristo ni uzinzi. Ni masheik wangapi wana ---- na kuzaana hovyo? Una akili lakini umeamua kuswitch off!
 
Umewagusa mpwa ngoja nisubiri salamu zao
 
ulianza vizuri sana.. Ila umeharisha vibaya unaposema ukristo ni uzinzi. Ni masheik wangapi wana ---- na kuzaana hovyo? Una akili lakini umeamua kuswitch off!
naomba usome vizuri post yangu. Kisha weka red pale nilipokosea
 
huzi huu ungekuwa unahusu kugegeda au mchepuko ungeona raia wamejaa kibao,ila mafunzo kama haya hawapendi kusikia mwisho wake wanaishia kujuta tu maishani,mkumbuke maisha ni sasa usikubali starehe ya muda mfupi iharibibu maisha yako.

Kuna watu wananiuzi sana umu wanakuja kujisifia kununua machangudoa,wengine wanafunza wenzao kuchuna mabuzi kwa kweli si poa,mnaaribu maisha yenu.

Tabia zibadilike mtoa mada yuko sahihi ila kwa vizuri ni huzi wa kuelemisha na kukanya uhovu utaona watu umu ingekuwa wanaruhusu watu kutoa ban ata mtoa mada ungepigwa ban na raia wa umu
 
Tunatakiwa tuache uzinzi siyo kwa sababu ya kuogopa kupata ukimwi bali kwa sababu ni dhambi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…