Uzinzi ni mbaya sana ukishaingia katikati ya watu wenye makubaliano ya kuoana

Uzinzi ni mbaya sana ukishaingia katikati ya watu wenye makubaliano ya kuoana

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
UZINZI ni NINI?
Imeandaliwa na
Magical power

Uzinzi
Ni tendo la kufanya mapenzi na mtu ambaye si mkeo au mume wako, na mara nyingi linachukuliwa kama kukiuka ahadi za ndoa au maadili ya kijamii...
NDOA ni yale makubaliano ya mwanamke na mwanaume kuingia katika mkataba(agano)litakalo husisha kuunganisha nyeti zao
Kutengeneza uzao na maongezeko kisha kuvuna baraka yake.

Dhana ya watu wengi hufikiri ndoa ni ile mchungaji na masheikh wanaweka mikono,huo ni mfumo wa taasisi tu,kuendelea kuwaweka watu wake,chini yao,kielimu na kimaslahi.
Kabla ya dini,ndoa zilikuwepo,
Kabla ya yesu ndoa zilikuwepo,kabla ya musa ndoa ilikuwepo...

Kuoana ni NINi?(marry )
Kuoana ni maana halisi ya muongiliano wa watu hawa jinsia mbili tofauti,,,,ndio maana kwa lugha ya kiingereza mwanaume anaweza sema will you marry me?
Akimaanisha utanioa?
Hivyo wote wanapokubali,wakiunganika kingono ndio kuoana...!

HII kauli kuoa
Kiuhalisia inatumika kwa wote mwanamke anaoa,mwanaume anaoa basi wawili hawa wakikubaliana kwa muingiliano wanaowana,..!

Sasa endapo mmoja wapo ataamua,kuipeleka nyeti yake ikaungane na mwingine kingono,
Hapo ndipo inahesabika kama UZINZI...

Uzinzi ni mbaya sana ukishaingia katikati ya watu wenye makubaliano ya kuowana,
Huwa ni gharama kubwa kuufuta,
Ni gharama kubwa kurejesha upendo na Amani ya awali,

KWA SHERIA HALISI ZA NAFSI Na ROHO,KUFUTA UOVU Na UNGANIKO lililoletwa na UZINZI ni mauti ya nafsi moja....
Umeona jinsi ilivyo hatari kwa huu, USHENZI.?

Nimekuandalia madhara na hasara zake kiroho kitamaduni.

Hasara za kiroho na kinafsi zinazohusiana na uzinzi zinaweza kuwa nyingi:

1. Hasara za Kiroho:
- Kukosa Amani ya Moyo: Watu wengi wanaofanya uzinzi hujiona katika hali ya lawama na hatia, ambayo inaweza kuathiri amani yao ya ndani.😎😎😎
- Uhusiano na Mungu: Katika baadhi ya tamaduni na imani, uzinzi unaweza kuathiri uhusiano wa mtu na Mungu au nguvu za kiroho, na kuleta hisia za kukosa kibali.
- Kujitenga na Maadili: Watu wanaweza kuhisi kuwa wanajitenga na maadili yao ya msingi, ambayo yanaweza kuathiri hali yao ya kiroho.

2. Hasara za Kinafsi:
- Matarajio na Uaminifu: Uzini unaweza kuharibu uaminifu kati ya wanandoa, na kusababisha kuvunjika kwa ndoa au uhusiano wa karibu.
- Madhara ya Kisaikolojia: Watu wanaofanya uzinzi wanaweza kupata hisia za huzuni, wasiwasi, na hata unyogovu kutokana na matokeo ya matendo yao.
- Kujitenga na Watu Wanaowapenda: Uzini mara nyingi huleta mgawanyiko katika familia na urafiki, na kusababisha watu kujitenga na wale wanaowapenda.

Kwa ujumla, uzinzi unaweza kuleta madhara makubwa ya kiroho na kinafsi, na ni muhimu kwa watu kufikiria athari za matendo yao kabla ya kufanya maamuzi kama hayo.......

UZINZI

Umefanya familia nyingi zimeharibika
Yaani baba haishi tena na mama,na watoto wakakosa nguvu thabiti wanabaki kuegemea upande mmoja.

Uzinzi
Umeleta mauwaji mengi yaliyozalishwa na uchungu,wa hesabu na gharama walizotumia wahusika juu ya wapendwa wao.😎

Uzinzi
Umeleta Aibu kubwa kwa watu,
Wengine walifikia kujiua,na kuacha vizazi vyao..

Uzinzi
Umewarithisha watu mikosi,laana,na mabalaa mengi.

Uzinzi
Umeleta watoto wasioeleweka katika nyumba maana kiroho ni watumwa,
Ni watu wa koo zingine,walioletwa utumwani kwa tamaa za mpuuzi mmoja aliyekosa uaminifu ndani ya nyumba...

Nina mengi ya kueleza
Ila kwa leo hili darasa nilifunge
 

Attachments

  • 1738498270712.jpg
    1738498270712.jpg
    248.7 KB · Views: 3
Uzinzi mtamu sanaaaa. Kwanza unakukutanisha na watu wengi

Pili unakufanya usake ndalama kwa nguvu

Tatu unasaidia ata wale sura mbaya wanawake wapate migegedo na sio kuchea kibomba

Nne uzi zi unasiadia kulisha famila maana arv zinapatika a kutokana na uzinzi. Ngo zimeajiri watu wwngi sana.

Tano husaidia kudumisha ndoa kwa kuwapa wahusika sehemu ya kujifunza style mupya mupya.

Inasaidia kukjza uchimi maana pombe condom hoteli bodaboda vinahusika.
 
Mbona andiko halijaandikwa ki professional Mkuu?
Uzinzi ni nini?
(...............)
Tafuta tafsiri nzuri ya Uzinzi.

Kufanya mapenzi ni kitendo cha watu wanaopendana na wakaona kufanya tendo.
 
Eti uzinzi nikufanya mapenzi namtu asiye Mumeo au mkeo!!!Kufanya mapenzi ndio nini? Otherwise mada ni nzuri.
 
Uzinzi mtamu sanaaaa. Kwanza unakukutanisha na watu wengi

Pili unakufanya usake ndalama kwa nguvu

Tatu unasaidia ata wale sura mbaya wanawake wapate migegedo na sio kuchea kibomba

Nne uzi zi unasiadia kulisha famila maana arv zinapatika a kutokana na uzinzi. Ngo zimeajiri watu wwngi sana.

Tano husaidia kudumisha ndoa kwa kuwapa wahusika sehemu ya kujifunza style mupya mupya.

Inasaidia kukjza uchimi maana pombe condom hoteli bodaboda vinahusika.
mimi Kama raisi wa ma jobless pro max, nasema una kitu ndani yako 😄😂
 
Kama una 18 mpaka 25 wewe zini tu tumia kinga kama 26 mpala 30 usicheezee maisha tafuta hela uoe au uolewa weka taratibu za maisha yako na sehemu. Yakipato vikojoleo vipo tu
 
Back
Top Bottom