Shemasi Jimmy
Member
- Apr 23, 2021
- 93
- 104
UZINZI WA OHOLA NA OHOLIBA, FUNZO KWA JAMII ZA WAKRISTO
Ohola (Samaria) na Oholiba (Yerusalem) binti za mama mmoja, wazinzi na waliogeuka chukizo mbele ya Mungu. Ni unabii wa Mungu uliotolewa kwa kinywa cha nabii Ezekieli (Eze 23:1-49)
Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Bwana Yesu apewe sifa wajoli wa Bwana. Ikiwa ni siku njema Bwana ametupa kibali cha kuiona siku hii ya leo, si kwa sababu sisi ni wema sana au wakamilifu bali ni kwa neema tu, basi sifa na utukufu apewe Mungu wa sszBwana wetu Yesu kristo.
Leo tutatazama jinsi mabinti wawili yaani Ohola (Israeli ama Samaria) na Oholiba (Yerusalem ama Yuda) na jinsi Mungu alivyowapenda na kisha wakazini (wakaacha njia ya Bwana) na kumuasi Mungu (Eze 23:4). Jinsi mambo haya yanavyoweza
Kuimarisha Imani yetu katika Zama hizi.
Mungu alipendezwa na Ibrahimu na kuahidi kuubariki ulimwengu wote kupitia uzao wake yaani Israeli (taz Mwa 12:3), Mungu alihaidi kuwatoa Israeli utumwani misri baada ya miaka 400(Mwa 15:13). Baada ya kutoka na kurithi nchi ya maziwa na asali, Israeli walimuasi Mungu na hatimaye wakagawanyika vipande viwili yaani Israeli (makabila 10) na Yuda (makabila 2). Kwa undani wa habari hii soma machapisho yaliopita.
Mungu akawaadhibu Israeli (OHOLA) Kwa makosa yao. Akawatia mkononi mwa Ashuru na hatimaye likatokea taifa la SAMARIA. Soma habari hii kwa undani katika machapisho yangu yaliopita.
Oholiba (Yuda) umbu lake ohola hakujifunza kwa yote yaliotokea kwa dada yake (Ohola) nayeye akaiacha njia ya Bwana na kugeuka chukizo kwa Mungu. Mungu akahaidi kuwapeleka uhamishoni babaeli Kwa miaka 70. Baada ya miaka 70 Mungu anawarudisha kupitia neno la Mfalme Koreshi wa Uajemi (Ezra 1:1-2) ili kwamba kristo azaliwe kupitia mabaki hayo.
FUNZO KWA WAKRISTO WA SASA
Maandiko yanasema:
Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
1 Wakorintho 10:11
Tunaona jinsi Israeli na Yuda (Ohola na oholiba)Mungu alivyowatia katika mikono ya mataifa maovu(Ashuru na Babeli) kutokana na uovu wao uliokithiri, isingekua utimilifu wa ahadi ya Mungu kwa Ibrahim(Mwa 12:3) Mungu angelifuta taifa hili katika uso wa dunia kama alivyofanya kwa mataifa mengine maovu.
Wakristo wa sasa lipo jambo la kujifunza kutoka katika uzinzi wa ohola na oholiba,Tazama jinsi Mungu alivyowapigania katika hali zote, lakini bado wakamuasi Mungu. Mungu anastahajabu ng’ombe na punda kua na hekima kuliko wana wa isreali kwa matendo yao(Isaya 1:3 SUV)
Wakristo tumeacha kujifunza mambo haya na kuyasahau,Leo hii kutenda dhambi imekua fahari, viongozi wa madhehebu ya kikristo wamekua sehemu ya kulitawanya kundi la Bwana badala ya kulikusanya na kulilisha hata Bwana ajapo. Wanatumia mimbari za Bwana kujihubiri wao na si kristo aliyetufia msalabani.Baadhi yao wamegeuza nyumba za ibada kua mapango ya walanguzi na hakuna wa kulisemea hili. Wewe uliye ndani ya kristo Ng’ang’ania neema ya Bwana uliyonayo, usiruhusu kutoka katika mikono ya Bwana,IMEANDIKWA: Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!(Ebr 10:31 BHN)
Ndugu zangu katika BWANA, ogopa sana dhambi kwa kua dhambi ni uasi, biblia inasema: Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi(1yoh 3:4) dhambi inatutenganisha na Muumba wetu.Mungu wetu ni mtakatifu hachangamani na dhambi yeyote. Acha dhambi sasa na mrejee muumba wako.
Mungu akubariki sana kwa kutumia muda wako wa thamani kusoma chapisho hili. Ukue na kuongezeka katika jina la Yesu!