Uzito uliopitiliza ni hatari kwa afya yako

Uzito uliopitiliza ni hatari kwa afya yako

Doctor MD

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
209
Reaction score
249
UZITO ULIOPITILIZA
Mgawanyo wa uzito kwa BMI hapa chini
Uzito ulio mdogo
<18.5

Uzito wa kawaida
18.5-24.9

Uzito uliozidi
25-29.9

Uzito uliopitiliza(obesity)
30-39.9

Uzito uliopitiliza na hatari zaidi


BMI
Huu ni mfumo wa ukokotoaji wa uzito wa mtu(KG) chini au ugawe kwa urefu wake(urefu zidisha kwa urefu)
Yaani BMI=uzito/urefu zidisha kwa urefu
Kizio chake =KG/M2

Uzito uliozidi huwa unapelekea chance ya kupunguza umri wa kuishi kwa Zaidi ya miaka 5 hadi 7 huu ni kutokana na utafiti uliofanyika. Sababu kubwa ni kutokana na kwamba uzito huathiri au hupelekea magonjwa mbalimbali katika mfumo wa kawaida wa binadamu.

Sababu zinazoweza kupelekea uzito kuzidi ni kama zifuatazo. Uwepo wa jeni za kurithi kutoka kwa wazazi kama vile baba au mama. Hii ina mana kwamba baba au mama wakiwa na uzito uliopitiliza basi watoto wao waweza kumbana na hiyo shida.

Aina ya maisha unayoishi kama vile kutokufanya kazi hii hupelekea sana kupata tatizo kama hili
Na aina ya chakula mtu anachokula haswa vile vinavyotengeneza sukari Zaidi ya 20 (rejea jedwali lenye aina mbalimbali ya vyakula)

UZITO ULIOZIDI= AINA YA VYAKULA UNAVYOKULA + JENI ZA KURITHI + MAISHA YA KUTOJISHUGULISHA
Tujaribu kuangazia jinsi mifumo ya mwili inavyoathirika kutokana na uzito uliozidi yani namanisha BMI >25(kubwa Zaidi ya 25)
 
Mfumo wa moyo, uzito uliozidi hupelekea
1. Shinikizo la damu
2. Kiharusi
3. Shambulio la moyo
4 Moyo kufeli kufanya kazi
5. Damu kuganda na kutengeneza mabonge madogo madogo ndani ya mishipa ya vein na kupelekea hiyo mishipa kuvimba, kupumua kwa shida n ahata kukohoa damu
6. Cholestrol kuzidi ndani ya mwili
 
Mfumo wa ngozi, uzito uliozidi hupelekea
1. Ndevu kwa wanawake
2. Michirizi ndani ya ngozi
3. Mwili kuvimba
4. Kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya ngozi
 
Mfumo wa Tezi, uzito uliozidi hupelekea
1. Mfumo wa hedhi kubadilika badilika
2 Mtoto kufia tumboni
3. Kisukari
4. Matatizo mbalimbali kipindi cha ujauzito
5. Utasa na ugumba
 
Mfumo wa chakula, uzito uliozidi hupelekea
1. Ubeuaji wa chakula kilicholiwa mara nyingi Zaidi na hali inayopelekea kupata shida ya upumuaji
2 Vijiwe ndani ya mfuko wa nyongo
3 Magonjwa mbalimbali ya ini
 
Mfumo wa ubongo, uzito huweza kupekekea
1. Kupoteza kumbukumbu
2. Kichwa kuuma kinachoambatana na macho kuuma
3. Kuongezeka shinikizo la damu ndani ya ubongo
4. Mfumo wa neva kuliwa ambapo huweza kupelekea Zaidi mwili ku paralyse
 
Mfumo wa upumuaji, uzito uliozidi hupelekea
1 Pumu
2. Upumuaji wa shida unaoambatana na kukoroma

Mfumo wa mkojo na kibofu, uzito uliozidi hupeleka
1. Matatizo ya nguvu za kiume
2 Figo kufeli kufanya kazi
3. Kukojoa kwa shida
4. Kwa watoto hupelekea kushindwa kuvunja ungo na kubalehe
 
Mifumo ya mifupa, uzito uliozidi hupelekea
1 Maungio kuuma sana
2 Maumivu chini ya mgongo
3. Gout

Mengineyo, uzito uliozidi hupelekea

1. Saratani
2. Mawazo mazito
 
Kesho panapo majaliwa ntaendelea na njia za kupunguza uzito
 
Shukran mkuu, hivyo vipimo vya urefu vipo kwenye unit ipi , namaanisha ni centimeter au meter ?
 
Hivyp vpo kwenye unit ya meter mkuu
Ukipata shida Zaid wasiliana nami
 
Nlifundishwa ukitaka kujua uzito wako wa mwisho kabisa chukua urefu wako in cm then toa 100 kinachobakia ndo uzito wako wa mwisho, ikizidi haya kg moja umeingia kwenye overweight.

Mf. Urefu wangu ni cm 175 nitafanya 175 -100=75. Hivo fanya ufanyavyo uzito wako wa juu usizidi 75kgs.
 
Nlifundishwa ukitaka kujua uzito wako wa mwisho kabisa chukua urefu wako in cm then toa 100 kinachobakia ndo uzito wako wa mwisho, ikizidi haya kg moja umeingia kwenye overweight
Mf. Urefu wangu ni cm 175 nitafanya 175 -100=75. Hivo fanya ufanyavyo uzito wako wa juu usizidi 75kgs.
Usfanye hvo mkuu Mana mtoto wa miaka 10 anawwza akawa na uzito uliopitiliza hvo ukifanya usemavyo utachanganya Mambo.

Kumbuka kutumia hzo standard kwa afya yako Bora zaidi kwa swali zaidi uliza
 
Back
Top Bottom