RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
💼 MHADHARA WA 11:
Hakikisha uzito wa VICOBA/au MICHEZO YA KUPEANA HELA unayocheza usizidi Mzani wa MFUKO (UCHUMI) wako. Kwa mfano upo kwenye uanachama wa VIKUNDI VYA MICHEZO YA KUPEANA HELA au VICOBA zaidi ya kimoja, halafu kila ifikapo muda wa marejesho ya madeni uliyokopa au muda wa kuweka hisa unapatwa na KICHAA CHA SAA 24, yaani huna raha ndani kwako - hiyo ni mbaya sana.
Kama utafanya biashara ambayo itakuwa inalipa madeni makubwa nje kuliko faida inayoingia ndani, ni lazima utafunga hiyo biashara - yaani hata ndoa yako utahisi inakupa kichefu chefu.
Kwa hiyo kama uzito wa VICOBA/au MICHEZO YA KUPEANA HELA itazidi Mzani wa MFUKO (UCHUMI) wako, au VICOBA unavyocheza hadhi yake iko juu haiendani na hali yako wala uchumi wako; ndugu yangu tegemea kutumbukia kwenye shimo la:
1. Msongo wa mawazo.
2. Kudanga - Ili kupata hela ya marejesho.
3. Kuuza assets zako muhimu kwa bei ya hasara (Mfano nyumba, Kiwanja, gari, duka, vitu vya ndani, n.k).
4. Kuikimbia nyumba yako - kutwa kushinda Bar au maskani ili kuwakwepa wahasibu wa Vicoba.
5. Ugomvi wa mara kwa mara kwenye ndoa yako, au kutengana kwenye ndoa.
6. Kumchukia mumeo/mkeo/mpenzi wako bila sababu ya msingi huku ukichukizwa na hali yake ya maisha.
By: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es Salaam,
Sept 20, 2024.
PIA SOMA
- Marejesho ya mikopo bubu na VICOBA yazidisha wimbi la wizi mjini na vijini