Uzoefu na Matumizi ya Additives za Kwenye Magari

Sanitaiza

Member
Joined
May 19, 2020
Posts
30
Reaction score
21
Wakuu,

Kwanza Eid Mubarak!

Naomba kujifunza kutoka kwenu Wakuu kuhusu additives za kuweka kwenye engine au gear box kwenye gari. Kwenye kausafiri kangu, naona kitu kama leakage kwa mbali kwenye gear box.

Hivi kuna ukweli kuwa nikiweka additive itazuia hiyo leakage? Sipendagi sana kufungua engine au gear box kwenye gari kwani ukirudishia haiwezi kuwa kama ilivyotoka kwa m-japan.

Na kama kuna mdau anajua additive nzuri ambayo itanisaidi, please naombeni msaada wa kuijua hapa kwenye hii thread.

Asanteni sana kwa mawazo yenu wakuu,

Eidd Mubarack
 
Hakuna manufacure ana entertain additives , ukishaenda upande huo jua unachukua risks peke yako. Kama ni leakage peke yake fungua hiyo gearbox utibu hilo tatizo kwa silicon ,

Sent
 
Zinafanya kazi, japo kiukweli mie huwa naziita temporary fix. Maana tatizo ni kama linabaki pale pale tu. Over time engine sealants zinachoka, uwezo wa kuvumilia oil pressure unapungua. Ni bora kutafuta fundi mzuri ukakagua leakage inatokea wapi. Mara nyingi unakuta ni oil seals au gaskets zimechoka tu. Ambazo replacement yake (isipokuwa kwa head gasket) sio complicated kivile kama fundi ana ujuzi na tools sahihi.
 
Sawa mkuu, nitafanya hayo, asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zinasaidia kwa mda mfupi tu ambao pengine tatizo limekukuta huna pesa Ila pia iwe additive ambayo ni genuine kabisa sio hizi ambazo zinatengenezwa rough na hazina ubora madhubuti sio mfanyakazi wa liquimoly ila bidhaa zao ni imara sana
Kwa ushauli wa vilainishi vya magari +255719263074
 
Asante mkuu kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…