Uzoefu wa biashara ya duka la madawa mhimu, jinsi ya kuendesha na changamoto.

aliyetegwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
313
Reaction score
486
Wanajukwaa naomba kwa wale wanaojihusisha na biashara ya duka la madawa mhimu wanisaidie ushauri jinsi ya kuendesha biashara hiyo, nimepata milioni tatu nataka kuanzisha biashara ambayo itanipatia vipesa vya kuendesha maisha kuna mdau nilimshirikisha akaniambia biashara hii naweza kutusua.

Sina uhakika kama milioni tatu inaweza kufanya marekebisho ya chumba na mtaji.
Mimi sio mtaalam wa kuuza madawa nitatakiwa kupata muuzaji, uendeshaji wa biashara utakuwaje, naweza vipi kucontrol wizi?
Anaweza asiibe lakini akawa anauza dawa zake mwisho wa siku akawa ananiambia biashara mbaya naweza vipi kuzuia hilo?

Faida za dawa zikoje, maana nahofu kubwa ya kupoteza ka mtaji kangu maana maisha yameshanipiga mnoo?

Ningependa kujua changamoto zote ninazoweza kukutana nazo katika biashara hii.
Muchango wako ni wathamani kubwa kwahakika utanitoa nilipo na kunipeleka sehem nyingine, shukurani.
 
Njoo na elfu 50 ni mtaji tosha kwa kuanzisha duka la dawa za mitishama.
Napatikana magu district kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…