Uzoefu wa Uingereza baada ya miaka mingi kubinafsisha huduma ya reli wameona kudolola kwa huduma huku nauli zikipanda bila uwiano. Nini somo kwa TRC?

Uzoefu wa Uingereza baada ya miaka mingi kubinafsisha huduma ya reli wameona kudolola kwa huduma huku nauli zikipanda bila uwiano. Nini somo kwa TRC?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Kama kawaida sekta binafsi huzengea uwekezaji za umma ili wao kuvuna faida badala ya umma kufaidika. TRC wameshatoa wazo la kubinafsisha huduma ya SGR, huku wakiwa wametaja makampuni yaliyo jitokeza yenyewe hata kabla ya kualikwa kutaka wao wapewe kuendesha. Sasa wao sijui ujuzi wamepata wapi au sio kwamba watawatumia wafanyikazi waliopo TRC na wao kuvuna peke yao gawio la faida ambalo ingebidi kwenda kwenye hazina ya taifa.

Usafiri wa reli ni rahisi kabisa kwa gharama za usafiri ardhini kwa kusafirisha tani moja kwa kilometa (ton/klm) kutokana na uzito unaoweza kubebwawa kwa safari moja. Safari moja ya treni inaweza kuchukua mzigo hata wa malori 100 au mabasi 100 ya abiria.

Ujenzi wa reli sio sawa na barabara kwa umri ambao mradi inabidi uwe hai bila ya tena kuhitaji kujengwa upya.
Nchi changa tumekua tunapelekeshwa na nchi za ulaya na marekani kufuana na maslahi binafsi ya makampuni yao ya kibepari. Kipindi cha Margarette Thatcheralipokua waziri mkuu wa Uingereza tuliambiwa lazima tubinafsishe huduma za umma kama usafiri wa abiria mijini, usafiri wa treni, huduma za maji na umeme kama walivyokua wameamua kufanya wao. Hii ni tofauti na jinsi wenyewe waingereza awali kwa miaka mingi walikua wakifanya kwamba huduma za umma kama usafiri wa mijini, treni, huduma za maji na umeme zitolewe na mashirika ya umma kwani mambo hayo yakiwa mikononi mwa makampunibinfsi wananchi wanaweza kulipizwa bei kubwa ambapo ni huduma za lazima kabisa kwa maisha ya kila mwananchi.

Hapa katikakati nchi yetu baada kusalimu amri kutokana na masharti ya mikopo na misaada toka nchi hizo za ulaya na Marekani tulibinafsisha huduma ya maji Dar es Salaam kwa kampuni ya Uingereza, tukaweka kampuni binafsi toka afrika kusini kuendesha Tanesco, na hatimae tulibinafsisha TRC kwa kampuni ya India, bila kusahau Air Tanzania ambayo tulibinafsisha kwa afrika ya kusini. Kote tulipata faida gani? Wawekezaji walilenga kupata wao tu wala sio kuimarisha huduma. Tulilizwa vibaya. Hapa sio mahali kueleza hasara ambayo nchi yetu ilpata. Ilikua ni wizi mtupu.

Hapa tumesikia serikali ya Labour uingereza wakizungumzia kuzorota kwa huduma ya reli kutokana na ubinafsishaji na sisi tunazungumzia kutaka kubinafsisha kile kimejengwa na fedha za umma kuwapa kampuni binafsi kuendesha. Uzoefu wa Uingereza makampuni binafsi wameendesha kwa maslahi yao tu. Kuna line za reli kule uingereza wamefunga huduma eti hazina faida japo wasafiri wapo. Wataam wa usafiri hufanyika cross subsidisation njia zenye faida kuendesha zile zinapata hasara ili wote kupewa huduma.

Kampuni binafsi wala hawawekezi zaidi ya kile umma wamewekeza wao wanataka kuvuna tu. Kwa hivyo Serikali sio kama hawajui nchi hii kuna uwezo na utaalam wa kutosha ila kuna wabinafsi kwenye uongozi wa taifa wataturudisha nyuma kwa kuwapa wageni kuendesha uwekezaji za umma kwa maslahi yao.
 
Kama kawaida sekta binafsi huzengea uwekezaji za umma ili wao kuvuna faida badala ya umma kufaidika. TRC wameshatoa wazo la kubinafsisha huduma ya SGR, huku wakiwa wametaja makampuni yaliyo jitokeza yenyewe hata m wa kutosha ila kuna wabinafsi kwenye uongozi wa taifa wataturudisha nyuma kwa kuwapa wageni kuendesha uwekezaji za umma kwa maslahi yao.
Serikali ya Tanzania haijawahi kufanikisha biashara yoyote angalia bus za muendo kasi, shirika la ndege, Tazara, nk.
 
Wamejifunza kwa mwendokasi hata wabinafishe sawa maadamu tupate huduma Bora.
 
Wabinafishe tren na sio reli mean wawape hata kampuni binafsi hata tatu ili zishindane kutoa huduma unachagua tu upande kampuni ipi, serikali haiwezi fanya biashara ibakie kupewa gawio tu.
Mbona vyoo vya serikali mfano mastand angalau vina huduma ridhisha kwa sababu ya ushindani.
Huku serikali ikipata gawio lake
 
Binafisha tu hata shirika la ndege nini faida zaidi ya hasara wana kila kitu lakini hawawezi kama mwendokasi.
Wapo radhi ndege iende nusu kwa sababu ya bei kubwa kwann usiweke bei ndogo ujaze siti zote na upate ruti nyingi kwa siku ili upate faida.
 
Back
Top Bottom