Uzoefu wangu kutegemea vyombo hivi vya Umma ni hatari kuliko hatari yenyewe

Uzoefu wangu kutegemea vyombo hivi vya Umma ni hatari kuliko hatari yenyewe

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mwaka fulani hapa Jijini Dar es salaam nikiwa naishi mitaa flani jirani yangu alipatwa na janga la moto. wakati tunapambana na huu moto jirani akawapigia simu zimamoto. tuliendelea kupambana na moto huo na baada ya muda mfupi (dk 50) walikuja zimamoto wakati huo kwa upande wa chini tumefanikiwa kudhibiti moto isipokuwa juu ya nyumba sababu ilikuwa hatuwezi fikisha maji kwa kumwaga kwa ndoo.

Jamaa walifika kwa mkwara sana na kutuondoa eneo hilo wakitaka kuanza shughuli ya uzimaji. angalau tukashukuru kuwa si haba...."heri kenda nenda kuliko kumi nenda rudi" jamaa wakato mpira wao mrefu mpaka kufikia eneo la nyumba. baada ya hapo wakaanza kuukunja tena kuurudisha kwenye gari. tukauliza inakuaje. wakasema walikuwa wanapima kama ule mpira unafika kwenye nyumba. wamegundua unafika sasa wanaenda kutafuta maji ya kuja kumwagilia. nakumbuka mwenye nyumba alienda kukaa chini ameinamisha kichwa.

Mbaya zaidi jamaa mmoja kati ya wale waliokuja na gari la zimamoto akauliza mwenye nyumba yupo wapi. akaoneshwa akamfuata na kumwambia ampatie tsh kama 50,000 hivi za kuwekea mafuta maana waliyo nayo hayatatosheleza kwenda na kurudi. mwenye nyumba aliangua kilio kama amefiwa. akainuka kumkunja jamaa tukamwahi na kumwambia waondoke na gari lao wasirudi tena. hili jambo lilitokea miaka kadhaa tu huko nyuma. na wananchi kadhaa walitaka kurusha mawe kuelekea lilipo gari tukawazuia sana wasifanye kitendo hicho.

Mwaka fulani nilikuwa mkoa fulani kikazi tukawa tumeenda kuonana na wadau flani wa hapo mjini. mara ikaja gari kasi ya wagonjwa kumchukua mgonjwa wakati huo tupo nyumbani kwa mwenyekiti wa Mtaa. na jirani alikuwa na mgonjwa ambaye amezidiwa anapaswa kupelekwa hosp ni mama mjamzito. Ilikuja hiyo gari na king'ora kwa mbwembwe nyingi sana. ukafunguliwa mlango nyuma ndani walikuwepo wauguzi/manesi watatu. Wamekaa tu kwenye mabenchi wakiwa wamevaa masks. raia wakawa wanahangaika kumbeba mgonjwa n.k wale wauguzi wamekaa tu wametulia wakipiga stories.lile gari lilikuwa na mabenchi tu pembeni katikatik hamna kitu so ikabidi wananchi wahangaike kwenda tafuta godoro. limepatikana godoro wale manesi wanauliza mwenye mgonjwa yu wapi? akaonane na dereva wamalizane kabla gari haijaondoka ili wakaongezee mafuta na kuziba pancha.

Hii ilikuwa hatari pia sababu muda uilipotezwa pale ulikuwa mkubwa ni bora hata mgonjwa angepelekwa hospitali kwa usafiri ninafsi.

So msishangae gari za zimamoto kufika kariakoo na kwenda kuchota maji uwanja wa ndege.... na washukuru angalau gari zilienda chota maji .sometimes unaweza kuta wale watu wa zimamoto wamepark gari hapo wapo busy ku chukua video gari yao inanguruma wakisubiri kupigiwa simu kuambiwa wapi kuna maji wakachote.
 
Nchi yetu inahitaji reformation kubwa sana Mana ujinga Bado ni kipaumbele kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom