Uzuri wa Diana na tamaa ya kwenda Ughaibuni vilivyomponza

Uzuri wa Diana na tamaa ya kwenda Ughaibuni vilivyomponza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Diana alikuwa binti mrembo sana mtaani kwao. Alishinda na bibi yake tangu akiwa mdogo, hii ilitokana na kuvunjika kwa ndoa ya wazazi wake na mama yake kurudi kwao Burma.

Vijana wengi walionyesha hisia zao za mapenzi kwa Diana. Mmoja wa vijana hao alikuwa James. James alizaliwa Scotland wakati wazazi wake wakiwa wanafunzi. Baada ya kumaliza chuo, James alimvisha Pete ya uchumba Diana kabla ya yeye kwenda Uingereza kuanza maisha akiwa na lengo la kumchukua Diana maisha yakiwa sawa.

James alikutana na changamoto nyingi alipoanza . Maisha hayakuwa mepesi kama alivyofikiria. Ilimchukua miaka mitatu mpaka kupata nyumba na nauli ya Diana. Kule nyumbani Diana alianza kusononeka kwani mawasiliano ya wakati huo yalikuwa ni ya barua na simu ya mezani. James hakuwa mzuri sana wa kuandika barua japo alitumia zawadi na pesa kwa Diana.

Mtaani alirudi David kutoka Marekani. David alisumbua mioyo ya wasichana wengi mtaani lakini roho yake ilitua kwa Diana. Diana alimueleza kuwa amechumbiwa, David alisema na yeye pia anaweza kuchumbia. David alimpeleka Diana kwenye mahoteli makubwa, walifanya picnics, walikwenda beach ilimradi tu Diana alichanganyikiwa.

Likizo ya David ilikwisha alimuacha Diana na mimba. Diana aliilea ile mimba, wiki anajifungia tu ndiyo James anarudi kutoka Uingereza. James alishapata habari zote, alikwenda nyumbani kwa kina Diana, Diana alitoka ndani mwenyewe. James alimpeleka ubalozini, Diana alipata viza. Walisafiri mpaka Heathrow. Walifika nyumbani salama Diana akiwa anamficha James hali halisi. James alimpa kipigo cha mbwa koko Diana na alimwambia arudi nyumbani kumfuta mtoto kwani anafahamu kila kitu.

James alimlea mtoto wa Diana kama wa kwake. Ingawa uhusiano ulivunjika baadae James alikuwa akimpiga Diana mara kwa mara. Mtoto alifahamu kuwa baba yake ni David na yuko Marekani. Mtoto alikuwa wa kike na sasa hivi ni mwanasheria. Diana alikutana na mtu mwingine aliyefunga nae ndoa yenye mapenzi. Uzuri wa Diana ulirudi kama awali na alipata watoto wawili kwenye ndoa mpya.
 
Hivi kwani mwanasheria naye Amechukua fomu?
 
Nilidhani unamsema mtu ninaemfahamu

Bahati nzuri Diana naemjua hajawahi panda hata ndege,
 
Huyu maza stori zake siziewagi kabisa..too hypothetical
 
Back
Top Bottom