Uchaguzi 2020 Uzuri wa kura ya siri

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Wiki ijayo tarehe 28/10 watanzania wote tunaenda kupiga kura kuchagua Rais, wabunge na madiwani

Jambo moja ambalo kila mmoja anapaswa alitambue ni kwamba kura yako ni siri yako.

Maana yake ni kwamba unaweza kuwa unampenda sana au ni rafiki wa karibu na Lissu lakini bado unaweza kumpigia kura yako Magufuli na wakati huo huo Lissu hawezi kujua kama umempigia kura Magufuli. Unaweza kufanya hivyo na bado urafiki wenu na Lissu ukaendelea bila hata matatizo unaweza kunywa nae hata chai, unaweza hata kumdanganya kuwa nimekupigia kura wewe na ukamshangilia na asijue, huo ndio uzuri wa kura ya siri.

Kura ya siri haina uadui wala ugomvi mpigie kura unayemuamini na urafiki wenu/wako bado utaendelea baada ya uchaguzi.

Kuna uwezekano mkubwa tarehe 28/10 Lissu akampigia kura Magufuli.

KURA NI SIRI YAKO
 
Uzuri wa kura ya siri haina ugomvi wala chuki,
kura ni siri yako na Mungu wako
 
kura ni siri yako hakuna atakaye jua uliye mpigia kura....hivyo unayo nafasi ya kufanya uchaguzi sahihi
 
Huo utakuwa ni usaluti na usaliti una kunyima amani na ni laana.
jambo baya ni kuisaliti nafsi yako, chagua unacho kiamini acha kuhofia, siasa sio dini.
kura ni siri yako mchague unaye muamini
 
kura ni siri yako keshokutwa yaani Jumatano twende tukampigie kura kiongozi unaye muamini kuwa atakuletea maendeleo na mwenye uwezo wa kutatua changamoto zinazo kukabili ktk eneo lako na taifa kwa ujumla.
 
And vice versa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…