Kama tunazungumzia mwonekano wa mwanamke, then mimi naamini beauty ni property ambayo ipo independent na mtizamaji (kama mtizamaji hajauona huo uzuri, haina maana haupo!).
Ni kama kwa mfano mtu ametoka kula muwa au nanasi na kisha aende kunywa chai, mara nyingi hata kama chai ina sukari nyingi, mnywaji atalalamika chai 'haina' sukari ya kutosha. Sasa, kimsingi hapa mnywaji hajaweza kutaste sukari iliyomo kwenye chai lakini hii haina maana kwamba chai haina sukari. Hapa ule 'utamu' wa chai ndio kama 'uzuri', kama upo, upo tu hata kama mtu fulani kwa wakati fulani hauoni.
Uzuri unahitaji kwa uchache vitu vitatu:
1. Mpangilio wa jumla wa viungo vyote vya mwili (composition), yaani kiungo kipi kimekaa wapi. Baina ya viungo kuna order yoyote? symmetry? assymetry?
2. Uhusiano wa size za viungo mbalimbali (proportion), mfano size ya kichwa ina uhusiano gani na kiwiliwili.
3. Umakini wa viungo mbalimabli (clarity), mfano kiwiliwili kieleweke kinaishia wapi na mapaja/miguu yanaanzia wapi? Vipi kuhusu rangi pia za viungo mbalimbali?