Uzuri wasababisha mke kupewa talaka

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088

Bwana mmoja raia wa Zimbabwe Arnold Masuka (40) ameacha watu vinywa wazi baada ya kuiambia Mahakama hamuhitaji tena mkewe Hilda Mleya (30) kwa sababu ni mzuri kupita kiasi.

Arnold mbele ya Jaji Henry Chizvidzo ametoa malalamiko hayo ambapo amesema ametoa talaka kutokana na kukosa usingizi kabisa kwa uzuri wa mkewe.

Anasema hali hiyo imemfanya imekuwa mbaya sana kwake kwani anaogopa hata kwenda kazini au kumuacha peke yake akiogopwa atawindwa na wanaume wengine.

Jaji amesema hii ni mara yake ya kwanza kusikiliza kesi ya aina hiyo.
 
Kaamua kujivua jakamoyo... Japo angejua hata akiwa mbaya uliwaji anaouogopa upo tu.
 
Hakuna kitu kibaya kama una mke na Bado una fikra mbovu kuwa unaweza chapiwa! Huwa ni kero hata kwa mke!!
 
mzabzab, jimbo limepoteza mbunge, mbunge kaona bora tu apige chini
 
The darker the berry the sweeter the juice!!
 
LIKUD aliwahi kushusha Uzi humu kuhusu hatari ya kumiliki mwanamke pisi Kali.Sio nzuri kuishi na mwanamke mrembo kupitiliza hata Mimi mwenyewe siwezi kbsa.

Aisee hutokaa uache kuwa na insecurities juu yake maana atakuwa anaziteka nyoyo za wanaume wengi na hapo kugongewa Ni dakika sifuri tu.
 
Kama ndiyo huyo kwenye picha sijaona uzuri wowote
Watu weusi tunaulimbukeni sana na Rangi asa uyo manzi ana uzuri Gani zaidi ya kuwa ana asili ya kiarabu Zibwabwe hakuna wanawake wa hivyo ndio maana anapagawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…