Kichwamoto
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 3,403
- 4,692
Habari za kutwa miamba na majabali ya jukwaa mujarabu.
Rejeeni kichwa cha maada, nimetafakari nyakati nyingi na kwa marudio kwanini nchi hii ina ombwe kisiasa,kidemokrasia na kikatiba.
Kwanini uhuru katika nyanja hizo si kipaumbele kwa Taifa hili?
Mara nyingi maswali yangu hujikita kitaaluma, sera mfanano za kidunia katika nyanja mbalimbali, mfano Bunge la muundo wa jumuiya ya madola, katiba kufuata muundo wa uingereza, kuwa na mfumo wa siasa za vyama vingi na miongozo yake.
Uhuru wa vyombo vya habari, uhuru binafsi wa mmoja mmoja wa kimawazo, maoni, ushauri na ukosoaji.
Katika nyanja zingine tunajinasibu kufanana na wengine mfano nchi majirani na ng'ambo, kwanini inapokuja kwenye mambo msingi na chocheo kimaendeleo na ukombozi wa kifikra katika taifa hasa siasa, demokrasia na kikatiba sio kipaumbele?
Je, mnufaika ni nani?ili iweje?na dira yake anaenda wapi?
Wanaotutaka tuwe mazuzu kwenye kila kitu, je, dira yao ni nini?
Tanzania ya Mazuzu haikubaliki.
Tupige vita uzuzu wa kulazimishwa.