Vanessa alazimishwa 'kudendeka' na shabiki

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


NJEMBA mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, juzikati aliwashangaza watu baada ya kulazimisha kudendeka jukwaani na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa akitumbuiza huku akipita kwa mashabiki na kutaka kuwapa mikono.

Katika hali ya kushangaza, Vanessa alipofika kwa mwanaume huyo alimpelekea mkono akitaka kumshika kidevu, ndipo njemba huyo alipomshika mwanadada huyo na kumvutia mdomoni mwake.
Hali hiyo ilimfanya Vanessa afurukute kujichomoa mikononi mwa mwanaume huyo na kuendelea na shoo huku akimuacha mshikaji akiwa kamtolea macho

Source: Bongo Movie
 
Anapiga shoo huku anahofia kuachwa !!!!!!!!!
 
Uki_zoom picha utaona hao walioingia humo kwenye show kama wapo kwenye zile free show, yaani hawana mzuka hata[emoji52] !!
 
Hiyo show mbona watu kama wana simanzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…