VAR kutumika msimu wa 2024/25 ligi kuu ya NBC

VAR kutumika msimu wa 2024/25 ligi kuu ya NBC

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Almas Kasongo amesema msimu ujao 24|25 Video Assistant Referee (VAR) itatumika ligi kuu.

Amesema, mfumo wa (VAR) utafungwa kwenye baadhi ya viwanja vinavyokidhi vigezo Nchini. Katika viwanja vya awali ni Benjamini Mkapa, Azam Complex, Mkwakwani Tanga na Majaliwa Stadium.

TELEMMGLPICT000167557528_trans_NvBQzQNjv4BqpVlberWd9EgFPZtcLiMQfyf2A9a6I9YchsjMeADBa08.jpeg
 
Ni jambo zuri. Ila na wale waamuzi wao vilaza wote ikiwezekana waachane nao. Maana wanatuharibia soka kupitia maamuzi yao ya kutatanisha.
 
VAR inaenda kuizika mazima kolowizard , si ajabu msimu ujao ikashuka daraja
 
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Almas Kasongo amesema msimu ujao 24|25 Video Assistant Referee (VAR) itatumika ligi kuu.

Amesema, mfumo wa (VAR) utafungwa kwenye baadhi ya viwanja vinavyokidhi vigezo Nchini. Katika viwanja vya awali ni Benjamini Mkapa, Azam Complex, Mkwakwani Tanga na Majaliwa Stadium.

View attachment 3009842
Je waamuzi wakiwa km waliokuwa wakiuchunguza mchezo wa yanga vs mamelody yaani wanao ahirisha kufikiri Kwa nafsi
 
Refarii Arajiga ataizima hiyo mpaka amalize ghorofa lake Chanika.
Nyie nao mnaboaaa! Makolo mmejaa nongwa , Arajiga hana baya, Kigoma mlishinda alipomtoa Mukoko alielipiza rafu ya mgongoni ya Boko, mbona mlipiga kimya hamkulalamika , basi Yanga kuibutua Azam kule Zenji na kubeba Kombe jingine mmeumiiiaaaa, na hasira zenu zote sasa kwa Arajiga!!

Arajiga ndie refa bora kwasasa bongo na hachezeshi kwa mihemko, au matakwa ya mtu au kumfurahisha mtu hasa nyie makolo tia maji tia maji, yaani Simba wote mlitaka Azam ishinde Zenji mpunguze uchungu na hilo halikuwa kwa maana Yanga ni next level, nyie mbona mlipigwa jumla saba na Yanga, sasa Azam wao wangewezaje!! Kwa vile Azam walibondwa makolo mkachukia sana na kuhamisha chuki kwa refa, naona mna kampeni haram ya kumtoa Arajiga mchezoni, na wala hana baya, hakuna mahali alikosea kuchezesha Zenji, mechi ya fainali huwezi kuchezesha kama unachezesha ndondo cup ile ligi yenu ya loosers aina ya shirikisho!!! Arajiga go go.

Dawa ni nyie makolo tengenezeni timu yenu acheni kusakama marefa wasio na makosa, acheni kulia lia, fanyeni usajili, la sivyo tutawakanda tena nje ndani au mnabisha? Kama vipi njooni na mpunga tuwape Ki Aziz
 
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Almas Kasongo amesema msimu ujao 24|25 Video Assistant Referee (VAR) itatumika ligi kuu.

Amesema, mfumo wa (VAR) utafungwa kwenye baadhi ya viwanja vinavyokidhi vigezo Nchini. Katika viwanja vya awali ni Benjamini Mkapa, Azam Complex, Mkwakwani Tanga na Majaliwa Stadium.

View attachment 3009842
Karia bana, Mkwakwani nao uwanja ule. Kule Ruangwa ni kujipendekeza tu kwa wanasiasa.
 
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Almas Kasongo amesema msimu ujao 24|25 Video Assistant Referee (VAR) itatumika ligi kuu.

Amesema, mfumo wa (VAR) utafungwa kwenye baadhi ya viwanja vinavyokidhi vigezo Nchini. Katika viwanja vya awali ni Benjamini Mkapa, Azam Complex, Mkwakwani Tanga na Majaliwa Stadium.

View attachment 3009842
Mpaka leo hatuoni VAR
 
Back
Top Bottom