VAR kuwekwa dimba la Benjamin Mkapa

VAR kuwekwa dimba la Benjamin Mkapa

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Note 📝
“Tutaweka chumba maalum cha Video za Marejeo (VAR) kitakachotumika wakati wote wa mashindano” sehemu ya maneno ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chanda akizungumzia ukarabati wa dimba la Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam.

72C71E62-C4CA-4F3F-B079-DB40C155864A.jpeg
 
Mambo mengi sana yanatakiwa kufanyika kwenye ule uwanja.

1. Viti vimepauka rangi
2. Nyasi kuboreshwa
3. Entrance ya VIP inabidi iwe tofauti na ya watu wa mzunguko
4. Vyoo kiujumla
5. Taa ni hafifu hazitoi mwanga wa kutosha
6. TV Screen ziongezwe
7. Audio System ya matangazo
8. Kuta zimechakaa
9. Sehemu za kueleweka za kununulia vinywaji na vyakula
10. Nje taa hazitoshi kuna giza mno
11. Mengineyo......
 
Hili wazo Mwigulu alikuwa kiongozi wake but alivyoona utopolo wanafaidi kwa kubebwa na waamuzi akaamua kufunga mdomo wake.
 
Hili wazo Mwigulu alikuwa kiongozi wake but alivyoona utopolo wanafaidi kwa kubebwa na waamuzi akaamua kufunga mdomo wake.
Hususani kipindi kile cha unbeaten ya mchongo
 
WAONGO sana Waliahidi Mwaka 2017 kuwa ifikapo 2021 watakuwa wamejenga uwanja mkubwa Wa kisasa Dodoma chini ya ufadhili wa Mfalme wa Morocco.

Mara tunajenga viwanja 8.

Mara tunaboresha Pitch.

NI UONGO MTUPU HAWAAMINIKI HAO WATU.
 
Afadhali pengine yale mabao ya makosa ya kibinadamu yatapungua kama si kumalizika.
 
Siyo kitu kipya kwa Simba labda hao wengine
 
Note [emoji404]
“Tutaweka chumba maalum cha Video za Marejeo (VAR) kitakachotumika wakati wote wa mashindano” sehemu ya maneno ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chanda akizungumzia ukarabati wa dimba la Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam.

#BenjaminMkapa #WizaraYaSanaa
View attachment 2560759
Kwa USHABIKI wa WAAMUZI wetu kwa Timu fulani fulani Mbona hata VAR watazichezesha zitoe matokeo Wayatakayo
 
Yaleyale tulioyasema kwenye ule uzi

Back
Top Bottom