VAR si ya kuichekea, inaharibu Soka

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Lengo la kuileta tech hii lilikua zuri isipokua kumekuwepo mapungufu au dosari katika mfumo huu, nini kilitakiwa

1) Var ilitakiwa iwe ina operate yenyewe kama mashine katika maamuzi kwa 95% ikishirikiana na mwamuzi wa Kati kwa 5%

2) Viatu vyote vya wachezaji pamoja na Lines zote uwanjani viwe installed na sensor,hata ikibidi wachezaji wavalishwe signals ili ikitokea mchezaji kawa offside mashine iwashe taa nyekundu na kumtaarifu refa direct kua ni off side kabla hata goli kuingia nyavuni au hata mchezaji haja shoot.

Warekebishe mambo hayo kulikoni ilivyo sasa goli linafungwa ati binadamu kwa utashi wao waamue kulihakiki au kukaushia, yaani kutegemea na mapenzi yao,au kwanza goli likifungwa wanaanza kuongea na refa muda mrefu kushauriana.

Hapo VAR inakosa maana kama wameamua VAR itumike basi zifanye kazi katika auto mode na si manual

Ifikie pahala VAR system ndio ituambie tena kwa haraka goli au si goli, Offside au sio offside, Faul au si foul, si kutumia watu wanne hivi ndio wawe wanaamua maamuzi mbaya zaidi mpira tunauona wote

Kiukweli VAR bila maboresho ni majanga. VAR ifanye kazi na refa direct.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes' Uko sahihi.

ila yakupasa utambue kuwa kila kifaa hutokea kwanza kwa maono ya awali, ndipo maboresho yanafanyika kutokana na mapungufu yajitokezayo, wakati kifaa kinapoanza kutumika katika uhalisia wenyewe.
 
sasa sehemu iliyopo mnataka iondoshwe. hapa tanzania haipo mnataka iletwe. mnachoitaka ni nini hasa
 
sasa sehemu iliyopo mnataka iondoshwe. hapa tanzania haipo mnataka iletwe. mnachoitaka ni nini hasa
Tatizo ni mapungufu yake yenyewe haina shida
Kuja kwa Var Tanzania na maeneo mengine ya dunia hilo nalo ni pungufu ambalo Fifa walirekebishe haraka
Kama Var inatumika Uk na Europe basi inabidi itumike dunia nzima ili kuweka uwiano sawa
Ligi moja kutumia Var nyingine kutotumia ni kasoro kubwa sana haijengi usawa baina ya timu zitumiazo Var na zisizotumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 

VAR ilipokuja waingereza wenyewe waliikataa. baada ya kuona magoli ya ofside yanakua mengi msimu wa pili wakaikubali na ikawepo. ni kweli ina challenge zake lakini ni toauti na ikiwa haipo, challenge yake kubwa ni kua mpira unapoa sana.
 
Mie Man U
Ila goli lile la pili la chelsea
Eti kiatu kimezidi
VAR
Isije Bongo aisee
Waiache kwanza
 
Kwa jinsi hiyo unayoongelea wewe itabidi hata referee na linesmen wasiwepo tena uwanjani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie Man U
Ila goli lile la pili la chelsea
Eti kiatu kimezidi
VAR
Isije Bongo aisee
Waiache kwanza

Magoli yale ya ujanja ujanja hayana nafasi, mbona mani U kafunga magoli mawili yote hakuna hata moja liliotishwa VAR, technologia inavyoanza siku zote wapo watu malibelari hupinga ila mimi binafsi naikubali, nikikumbuka mwaka 2010 world cup kule S.A lampard anapiga mzinga moja hatari wakati wako nyuma bao 2 kwa moja ilikuwa comeback ya hatari mpira unagonga besela unadundia ndani manuel neur anatoa refa anapeta. Ule ulikuwa ni uonevu na makosa ambayo sasa VAR umekuwa mwarobaini. Sisi waafrica hatuna tunachoweza zaidi ya kusubiri wazungu wateletee tupokee kwa kupinga kwanza badae ndio tunapenda. Wakati gari za auto zinaingia TZ watu walikataa kabsa na kusema za kike lakini sasa kila kitu kipo wazi.
 
Umeongelea vitu visivyowezekana
Hakuna namna binadamu lazima wahusike
 
Bahati pia ipo kwenye soka, kama mchezajivkafunga goli tata na refa hajaona hiyo ni sehemu ya mchezo....VAR ukizidi hata kiatu ni offside.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…