JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Imeripotiwa kuwa mashine maalum ya VAR (Video Assistant Referee) iliyokuwa imewekwa Abuja Nigeria kwa ajili ya kusaidia waamuzi wa mchezo wa play off wa kufuzu Kombe la Dunia 2022 kati ya wenyeji Nigeria dhidi ya Ghana imeibiwa uwanjani hapo.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare bao 1-1 ambapo faida ya bao la ugenini likaipa nafasi Ghana kufuzu. Vurugu ziliibuka kwa mashabiki wa Nigeria kuingia uwanjani baada ya matokeo kutokuwa rafiki.
Mapema leo Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limetangaza kuufungia uwanja huo wa MKO Abiola uliopo Abuja kutokuchezwa kwa michuano/mechi za kimataifa.
Source: Ghpage