Samahani sana kwa wale wenye kutawaliwa na jaziba.
naomba nijibiwe swala langu hili linalonisumbua. Toka nizaliwe mpaka leo kila nionapo picha ya Bikra maria huwa naona vazi lake ni Hijabu, lakini nikiiangalia jamii ya wakristo sioni wanawake zao kujipamba kwa mithili ya mavazi ya Bikra maria.
1.swali ivi ni kwanini wanawake wakristo hawavai kama alivyokuwa anavaa bikra maria?
2.Je ma sister kuvaa vile wavaavyo ipi reference yao? and why not for other kristian woman?
mavazi ni tamaduni za eneo husika, angekuwa amezaliwa umasaini akavaa lubega unataka wanawake wote wavae lubega?
Pia hakuna mahali palipoandikwa wanawake wavae kama bikira maria......ila wanawake wanatakiwa wavae kwa kujisitiri kwa hiyo ukivaa gauni lako lililokufunika vyema inatosha.
Halafu wakristo hawaongozwi /kutambuliwa kwa mavazi....
Msihangaike kusafisha kikombe kwa nje wakati ndani kimejaa uchafu,...... bali kikombe kisafishwe ndani kwanza then nje........ Roho kwanza then mavazi........