Vazi La Diamond Platinumz Lililochangia Kupigwa Marufuku Video Ya Dully Sykes

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Wote tumemsikia jana Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa kwa video yake ya kabinti special na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu mbili zilizosababisha video hii kufungiwa na ya kwanza ni kitendo cha msanii Diamond Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno ambalo ni tusi .

Hii ingekua kwa nchi za mbele basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu kinaitwa "blurring" yaani
wanayafanya maneno yasisomeke lakini wabongo wakaona isiwe tabu na director akaamua kuacha video irushwe ikiwa katika hali hii.Sababu ya pili ni vazi la ufukwe yule demu alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua mbaya.


Je, Unadhani ni haki video hii kufungiwa na kama ni haki je unafikiri ifungiwe ni kwasababu ipi ya msingi?


 
Na huyo binti aliyevaa nguo za mdani tu hakuchangia kufungiwa kwa video?
 
Dah asee mi naona mavaz ya uyo dada ndo yaweza kuwa sababu kuu ya kusitishwa iyo video
 
Ni haki kabisa huyu dada kavaa nguo zisizoendana na utamaduni wetu.
 
Masikini jaman Wangemuuliza kama Diamond anaelewa maana ya Maneno yale!
Maana english thee eee since am children theee
 
BASATA nitaandaa makala maalum Mungu akijalia kuwaunga mkono ktk juhudi hizi.Hatuwezi kuishi tu bila misingi na heshima ya tungo na staha za hawa wasanii wanaochukuliwa kama role model na watoto wetu.

Leo nakuunga mkono,na sio hiyo tu kuna video nyingi sana movie nyingi hata matangazo ya TV na radio yapo mengi sana yasio na maadili hata chembe,sijui tunalea au kuunda taifa gani huko mbeleni
 
Domo bana toka ajue kiswanglish tabu sanaaa

Yote hayo dadaangu ni kwa sababu ya ULIMBUKENI...wabongo wangi wanapenda sana artificial life,Kuiga lifestyle tusojua nini mwisho wake.

Yani huyu Domo nadhani haezi enda fanya show Uganda tena,coz upuuzi kama huu umeshazikwa juzi na Mhe.Museveni
 
Mi nashindwa hata kuelewa wanakata za kibongo lkn za America wanapiga na kuzirusha live.
 
Dully alihojiwa aliongea pumba tupu. Eti wasanii wanaongeza pato la Taifa kwa hiyo nchi isiwabane na video kama hizo ndo zinafanya wawe stars. Anasema nchi yake badala imsupport sasa ndo ina mdidimiza kimaendeo.
Kwangu nimeona hana lolote yeye afanye mazuri then support ataipata.
 
Hivi bila kumtaja Diamond Matak.o yenu yanawasha?

Hahahahaha sasa Matola ndio nini hivi hujui siku hizi mie rafiki yangu invisible,ntakuchongeaa
We uliambiwa uweke picha yako hujaweka acha tumjadili domo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…