VAZI LA WAZIRI MKUU WA FIJI LAZUA GUNZO..!!

VAZI LA WAZIRI MKUU WA FIJI LAZUA GUNZO..!!

kiben10

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
613
Reaction score
791
Habari ndio hii jioni kutoka BBC, Wakenya wengi kutoka kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi.

Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.

Je na wewe umepigwa na humuelewi?
bbcswahili-20190530-0001.jpeg
 
Hata mume WA princess Diana nilishaona kwenye TV kavaa sketi yenye rinda box ya draft. Tena zaidi ya mara moja
Ni Scottish traditional garment inaitwa kilt, full garment inaendana na rubega la kimaasai.

images
 
Nchi fulani katika sherehe za Idd kukawa na mjumuiko wa Watanzania, wengi walikuja wamevaa makanzu lakini wenyeji waliokuwepo hapo kwenye hiyo 'shughuli' hawakuwashangaa ila kazi ilikuwa kwa wale waliokuwa wamevaa misuli, seriously kuna jamaa aliniuliza kama hiyo ilikuwa ni sherehe ya kidini mbona kuna wanao'display ushoga waziwazi kwa kuvaa mavazi ya kike.
Niliishia kucheka tu, kila watu na tamaduni zao.
 
Back
Top Bottom