Uchaguzi 2020 Viapo vya mawakala

Madhara ya vyama kutojiandaa ndiyo haya

Ufafanuzi huu ni kwa mujibu wa kifungu cha 57 (1) na (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na kifungu cha 58 (1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292

Chama cha siasa kinaruhusiwa baada ya kupata ridhaa ya Mgombea au Wagombea kuteua na kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi orodha ya majina ya mawakala wa upigaji kura siku saba (7) kabla ya siku ya uchaguzi

Ni vema mawakala wapangiwe vituo vya kupigia kura ndani ya kata wanayoishi ili waweze kuwatambua wapiga kura.

Kila chama cha siasa kitakuwa na wakala mmoja tu kwa kituo ambaye atawakilisha wagombea wa chama hicho kwa uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani katika kituo husika

Utambulisho wa Mawakala wa Vyama Vya Siasa

Kwa mujibu wa kanuni ya 50 (6) ya Kanuni Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 43 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020, barua ya utambulisho wa kila wakala itakayowasilishwa na chama iainishe kituo alichopangiwa na iambatishwe na picha mbili (passport size) zilizopigwa si zaidi ya miezi mitatu.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu 57 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 chama kitaruhusiwa kuteua wakala mbadala endapo aliyeteuliwa awali amefariki au ameshindwa kutekeleza majukumu ya uwakala. Katika kurahisisha utekelezaji wa suala hili, sambamba na orodha ya mawakala wa vituoni, vyama viwasilishe majina mawili ya mawakala wa ziada kwa kila kata ambao watatumika kama mawakala mbadala iwapo itahitajika

Endapo wakala hana picha anaweza kuwasilisha nakala mbili za mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo: -

(i) Kadi ya mpiga kura;

(ii) Kitambulisho cha Taifa;

(iii) Leseni ya udereva; au

(iv) Pasi ya kusafiria. Baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kupokea utambulisho wa mawakala atafanya yafuatayo: -

(i) Ataandaa orodha ya mawakala kwa kila kituo.
(ii) Ataikabidhi orodha hiyo kwa Wasimamizi wa vituo pamoja na barua ya utambulisho yenye picha wakati wa kugawa vifaa. Kama barua haina picha iambatishwe na moja ya nakala za vitambulisho vilivyotajwa hapo juu.
(iii) Atawaelekeza Wasimamizi wa Vituo kubandika orodha ya mawakala watakayopatiwa nje ya kituo cha kupigia kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura.
(iv) Atawaelekeza Wasimamizi wa Vituo wasiombe utambulisho mwingine wowote kutoka kwa mawakala wa vyama. Tume inashauri uteuzi wa mawakala uzingatie uwiano wa kijinsi na makundi maalum kama vile vijana na watu walemavu.

Hata hivyo, vyama vya siasa vina mamlaka kamili juu ya uamuzi wa kuteua mawakala kwa kadri watakavyoona inafaa.
 
..yani ndio unajiuliza wakati hii hujuma inafanywa sheria wabunge walikua hawaoni??na hii ilitakiwa iwe issue ya kampeni..kwamba wabunge wa ccm ndio wamepitisha sheria hizi za hujma .....sasa nakala zipungueje wakati tume imepewa pesa nyingi na serikali kwasababu ya uchaguzi??...hamna namna ya kukubali huu upuuzi....nakala hata kama mawakala watakua milioni lazima zitoshe...hela si zilitolewa kwa ajili ya kuandaa uchaguzi!
 

Mtazamo wako Ni sahihi kabisa Ndugu Mtanzania. Uchaguzi huu ni wa kufa au kupona. Hilo angalizo lako linatakiwa lifanyiwe kazi upesi.
CHADEMA na ACT Wazalendo tafuteni Mawakala WAAMINIFU wenye IDs(NIDA, MPIGA KURA, PASSPORT, LESENI) zinazosomeka majina kikamilifu otherwise NEC NA WASIMAMIZI toka CCM(Wakurugenzi) wanakwenda kutumia hiyo kama loophole ya kuwa disqualify Mawakala wenu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…