Viapo vya ndoa....nyongeza

pinkmousse

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
227
Reaction score
88
Habari zenyu ndugu zangu,eti kwenye viapo vyetu vya ndoa hamuoni busara wakiongeza maneno yafuatayo: "sitaacha usiku upite nikiwa na hasira juu yako". Nimeona tu kwamba mara nyingi wanandoa mkilala mmekasirikiana bila kusameheana kunazidisha hasira na mipasuko kuimarika na wakati mwingine kupelekea ndoa kuvunjika. Wenzangu mnasemaje?,nawaza tu kwa sauti kuu..weekend njema!
 
Pale kwenye Nitakupenda pamebeba yote,huwezi kuwa na hasira ya miezi kama una UPENDO
 
Nilienda kwenye ndoa ATN church,aisee kiapo kigumu! Nt exact words, ila 'sitajishughulisha na mwingine yeyote ila wewe tu, sitakufanyia vituko, sitakusumbua, nitakuheshimu na kukupenda...', sina hakika nadhani nilipoteza fahamu sikusikia mwisho wa viapo
 
mwambie kulala na hasira haivutii, ndo mwanzo wa kunyimwa huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…