Mr_mkisi
Member
- Sep 24, 2024
- 15
- 47
Unajisikiaje, unatafuta pesa mingi na Kujikusanya alafu mtu anakuja kukuibia Kirahisi tu.
Inaumiza eeh!
Hivi karibuni nimekuwa nikipata malalamiko mengi kutoka kila kona ya Tanzania.
Hapa naamanisha unaweza kuipenda bidhaa fulani wewe upo mkoa A na unamtumia muuzaji mkoa B alafu baada ya kutuma pesa anapotea.
Kama kawaida, mwanenu ninaye wakubali ikabidi niingie mzigoni, nijue Nini kinasababisha wengi kudhulumiwa.
Na hizi ni dalili / Viashiria 6 kuwa utapigwa ukimtumia pesa.
1. Haonyeshi sura yake
Mfano, haweki profile picha kwenye mitandao yake ya kijamii na humuoni akiposti video zikionyesha sura yake akinadi / kuelezea bidhaa zake au kurekodi tu video za kawaida. Kuwa makini.
2. Haposti Mara kwa Mara/ Post Chache
Unakutana na page mfano FB ,au Instagram yake haposti mara nyingi labda unakutana na posti ya mwisho ina miezi 2 kurudi nyuma. Kuwa makini.
3. Anafunga Comment
Hapa angalia zaidi kwenye tangazo lake analo post ukiona mtangazaji anafunga comment kuna asilimia kubwa kuwa sio muaminifu hii inaweza kuwa kwenye Tangazo analo lipia au post zake nyingine za nyuma.
4. Ni Ngumu kufikika
Wauzaji matapeli wengi hutangaza wapo maeneo ambayo ni ngumu kufikika kwa kawaida ili uwe na chaguo moja tu la kuwatumia pesa na mara nyingine huweka Vikwazo vingi unapo onesha nia ya kumfuata alipo.
5. Bei ndogo kupindukia
Hapa naongea na wewe unayependa kitonga 😅. Naona unacheka
Soko la bidhaa nyingi huwa bei zake hazitofautiani sana kati ya muuzaji mmoja na mwingine.
Ukiona mtu anauza bei rahisi kupita kawaida, stuka unapigwa ni vyema kufanya research juu ya bei ya bidhaa husika📌
6. Pesa Nusu
Ukikutana na mfanya biashara anasema ulipie pesa nusu kisha nyingine umalizie mzigo ukifika KUWA MAKINI.
Mfanya biashara serious, ni lazima utume pesa yote ya mzigo ndipo utumiwe bidhaa au kwa yule unaye lipia baada ya kupokea wengi huomba nauli kisha ukipokea mzigo unalipia bidhaa yako.
Hapo wengi hudai ulipie pesa nusu ukimtumia atadai umalizie ndipo akutumie ukikataa inamaana pesa yako itakuw imepotea na ukimalizia ndipo anapotea mazima.