Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Dharau huwa zinajitokeza kwa Watu wengi pale ambapo wanakuona hauna pa kwenda,pale ambapo unaonyesha kuwahitaji sana ili uwe na furaha.
Unapokuwa mpweke kupitiliza,unapokuwa hauna furaha utalazimika kutumia fedha nyingi sana, nguvu nyingi sana,juhudi kubwa sana ili upate ukaribu na mwanaume au mwanamke ûnampenda sana lakini udhaifu wa utaratibu huo ni kwamba mtu yeyote akiona unamuhitaji sana anaanza kukudharau kwa makusudi kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Ni vema kuishi na mtu yeyote kwa muktadha wa kumtegemeana (interdependence) kwa maana wewe uwe unahitaji uwepo wake na yeye awe anahitaji uwepo wako sio yeye kuonekana ni super star kisha wewe uonekane kama shabiki wake.
Kuheshimiana , kuwasiliana kwa lugha nyepesi,fasaha na yenye kueleweka ndiyo msingi wa mahusiano imara , vilevile dharau, majivuno, kiburi, ujuaji, ubishi, utemi ,ubabe , ukatili, udikteta, udhalilishaji,ukali kupitiliza huwa chanzo cha mahusiano kuvunjika hata kama yamekuwa imara kwa muda mrefu sana.
Viashiria kwamba unatakiwa kuachana na Mwenza wako ni
1.UNATAKA KUMBADILISHA TABIA
Kama unaona mwenza wako yupo na tabia ambazo hazifai katika jamii lakini wewe ndiye ambaye hauna amani kwa sababu ya tabia zake kwa maana wewe unahangaika kumbadilisha tabia kila siku bila mafanikio yoyote na unatafuta ushauri na mbinu za kumfanya akupende sana kuliko mtu yeyote.
Unaweza kutaka kumbadilisha tabia kama vile unajua ni mlevi kupindukia unataka aache pombe,unajua yupo na tabia sugu kama kucheza kamari, wizi, uhalifu,anakusaliti mara kwa mara,unajua mwenza wako anadaiwa fedha kila kona lakini unajitoa mhanga kulipa madeni yake yote,unajua hataki kazi lakini unatafuta kazi kila siku,unajua hawezi biashara unampa mtaji anakula kisha anakufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi muonekano wako lakini unataka kujitoa mhanga katika maisha yake.
2.UNAVUMILIA TABIA AMBAZO HAUZIPENDI WALA HUWEZI KUVUMILIA KWA WATU WENGINE
Mwenza wako hawezi kupiga simu ila wewe unapiga mara kwa mara, anaweza kukaa kimya muda mrefu sana bila kukupa taarifa yoyote kisha ukianza kumtoa kichwani anakuja kwa kasi sana anapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo,kuonyesha upendo sana kisha ukianza kuonyesha kumpenda sana anakata mawasiliano moja kwa moja anakaa kimya sana wiki, wiki mbili, mwezi bila taarifa yoyote lakini kila akija kwako unampa nafasi nyingine.
Akiwa na shida anakuja kwako kuomba msaada kisha shida zake zikiisha anaondoka zake hakuna mawasiliano yoyote mpaka akiwa na shida nyingine anakuja kwako tena.
Unajisikia furaha ukijitoa mhanga kumsaidia mara kwa mara kama hauna kitu chochote cha kumpa unahisi hawezi kukupenda.
Huwezi kumuomba msaada wa kitu chochote kwa sababu unaogopa atakasirika lakini unazidi kujitoa mhanga kwake ukiamini atakuja kubadilika lakini haonekani kujali chochote.
3.UNAAMINI HUWEZI KUISHI BILA YEYE
Mara kwa mara unahisi upweke kupita kiasi kama yupo mbali na unajisikia vibaya sana mwilini ikiwemo moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu, miguu kuishiwa nguvu, tumbo kuvurugika, kuumia kooni, kutetemeka sana, kutokwa jasho viganjani, kutamani kumdhuru, kumuombea mabaya kimyakimya, kumchukia kisirisiri, hasira kupita kiasi,kujiona haupendezi ukivaa nguo yoyote, kujiona mbaya sana wa muonekano,kujiona mkosaji muda wote,kujiona takataka mbele ya jamii kisha yeye unamuona mzuri sana hana dosari yoyote na unahisi mkiachana huwezi kupata mwenza mzuri kama yeye ila unahisi yeye atapata mwenza mzuri kuliko wewe.
Hivyo mara kwa mara unambembeleza sana aonyeshe KUKUPENDA lakini hajali kabisa hisia zako na hauna hisia zozote kwa watu wengine wenye kuonyesha kukupenda sana na kukujali.
Mtu yeyote akionyesha kukupenda sana unapoteza hisia juu yake.
4.MUDA WOTE UNAFIKIRIA NJIA ZA KUMFURAHISHA LAKINI YEYE HAJAWAHI KUFANYA HIVYO KWAKO
Mara kwa mara unafikiria kumnunulia zawadi,kumpa fedha,kumpa ushauri,kujishusha sana, kumnyenyekea sana,kuepuka kumkasirisha muda,kuongea kwa umakini sana lakini anaibua ugomvi mara kwa mara.
Kila wakati unajiona upo na dosari nyingi sana kwanzia muonekano, lafudhi, vipaumbele vyako,malengo yako, historia yako, familia yako lakini yeye unamuona mzuri sana hana dosari yoyote na mara kwa mara unaogopa hasira zake.
Akikuomba kitu chochote ukisema huna anakuchukia moja kwa moja kisha unaanza wewe kumuomba msamaha,akifanya makosa ukihoji makosa yake anageuza kibao kwako kisha anakaa kimya sana muda wote kisha unamuomba msamaha kwa makosa yake mwenyewe.
5.KAMA MWENZA WAKO AKIWA NA HASIRA TU UNAANZA KUJILAUMU MWENYEWE
Mara kwa mara unajenga hofu ya kurudi nyumbani kwa kuhofia "mood" gani utamkuta nayo.
Mara kwa mara unakaa kimya bila kuongea kitu chochote ili kuepuka ugomvi baina yenu,mara kwa mara anakufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi muonekano wako,anadai hauna hadhi ya kuwa na yeye lakini huwezi kumuacha kwa sababu amesema mkiachana hakuna mtu yeyote ambaye anaweza KUKUPENDA zaidi yake na wewe anaishi na wewe kama kukusaidia kwa sababu hakuna mtu yeyote ambaye anaweza KUKUPENDA kwa hivyo ulivyo.
6.MUDA WOTE UPO TAYARI KUMFURAHISHA HATA KWA KUACHA SHUGHULI ZAKO ILA YEYE HAWEZI KUFANYA HIVYO
Mara kwa mara anasema uongo na kukataa ukweli kwa makusudi lakini bado unajitoa mhanga kwake kumfurahisha lakini yeye hawezi kufanya hivyo kwako hata ukiwa mgonjwa mahututi.
Hata kama upo na kazi ngumu sana upo tayari kuacha kazi kwa ajili yake lakini yeye hawezi kuacha kazi , vilevile hata kama hana kazi yoyote hawezi kujitoa kwako kwa jambo lolote.
7.KAMA KUMETOKEA UGOMVI WEWE NDIYO UNATAKA KUSULUHISHA TU YEYE HATAKI
Kama amefanya makosa ukianza kuzungumza makosa yake anakuwa na hasira kupita kiasi,anakuwa mkali sana, anakufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi maelezo yako,kuongea uongo kwa makusudi kisha anabamiza mlango na kuondoka zake.
Mara kwa mara unakata tamaa juu ya msimamo wako ili kuruhusu amani baina yenu.
Mara kwa mara unakubali kubeba lawama juu ya makosa yake mwenyewe.
8.KAMA UNAMUHITAJI ANAKUWA BUSY SANA LAKINI WEWE HUWEZI KUJIZUIA
Kama mwenza wako akiwa na shida ya fedha unajitoa mhanga haraka,akitaka mapenzi unajitoa mhanga haraka, lakini siku ukiwa na shida yoyote hawezi kujitoa kwako hata kama uwezo wa kufanya hivyo upo utaona anatafuta kisingizio cha kuondoka, ukilalamika tabia zake anakuwa mkali kupita kiasi na ananuna muda mrefu sana mpaka unaomba msamaha wewe kwa makosa yake.
Akiwa na shida yoyote anaonyesha kukupenda sana lakini ukimpa mahitaji yake tu anapoteza hisia juu yako na anaondoka zake
Akiwa na shida anataka kuja kwako lakini ukitaka ukaribu naye anakuwa na hasira kupita kiasi na dharura za mara kwa mara.
Ukianza kuzungumza kuhusu matatizo yako binafsi anatazama pembeni lakini akiwa na shida anataka uache kazi zako zote umpe mahitaji yake kisha ukimaliza anaondoka zake mpaka akiwa na shida tena.
VYANZO VYA MWENZA WAKO KUONYESHA KUKUPUUZA SANA UKIMUHITAJI NI
Vyanzo vya tabia zake ni hivi vifuatavyo
1.SABABU ZA HIVI KARIBUNI
I.Amevunja mahusiano yake na mwenza wake ambapo bado anampenda sana Mwenza wake na hawezi kumtoa kichwani
II.Anaogopa kuumizwa sana kama atajenga mahusiano ya karibu sana na wewe
III.Anaogopa kuonyesha hisia kali za mapenzi kwako anahisi utamuona DHAIFU SANA
IV.Anataka kujenga mahusiano ya juu juu na wanawake au wanaume wengi sana kwa wakati mmoja
V.Anaweza kuwa na mwenza wake ambaye anampenda sana ila anafanya siri usijue kama anasaliti
SABABU ZA UTOTONI
MALEZI YA UTOTONI MWAKE
Mwenza wako atakuwa amepitia malezi ya namna hii utotoni
1.UPENDELEO KUPITA KIASI
Atakuwa anatokea familia ambazo tangu utotoni mwake amekuwa anapewa upendeleo kupita kiasi ndani ya familia kwa maana baba au mama yake mzazi hakuna mwenye uwezo wa kumuonya kwa jambo lolote.
Kwa maana yangu utotoni amekuwa akiwa huru kula chochote, kuvaa nguo yoyote,kwenda sehemu yoyote,amezoea kunyenyekewa tu na kuombwa msamaha hajui kujishusha kwa mtu yeyote hivyo hawezi kubadilika hata ufanye nini.
2.ADHABU KUPITA KIASI
Kama anaonekana yupo na tabia ya ukosoaji kupita kiasi,hasira kupita kiasi,ubabe sana atakuwa amezoea kupigwa sana, kutukanwa, kufokewa, kubaguliwa, kuzomewa, kugombezwa sana,kulazwa chooni, kumwagiwa maji, kufukuzwa nyumbani, kunyimwa chakula, kunyimwa mahitaji,kupigwa ngumi, kupigwa vibao usoni,kupigwa nyaya za umeme, kuburuzwa chini, kugeuzwa kichwa chini miguu juu, kuzuiwa kwenda chooni muda mrefu,kukabwa shingoni.
Hivyo atarejea tabia zilezile za utotoni mwake.
3.UPWEKE KUPITA KIASI
Anaweza kuonekana hivyo kwa sababu ya kumbukumbu za upweke kupita kiasi kwa njia zifuatazo
Talaka au kutengana kwa wazazi,ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi, kifo cha mzazi, wazazi kutengana na kurejeana mara kwa mara, kulelewa na watu wengi sana mfululizo,kuishi bila kumjua baba au mama yake mzazi
tangu utotoni.