olimpio
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 418
- 866
Tarehe 21 Feb ,ICT commission ilitoa tuzo muhimu tatu kwa kampuni ya YAS(zamani Tigo)
Walishinda Tuzo tatu kama zilivyo hapa chini
1. Huduma Bora za Intaneti (Best Internet Service Provider)
2. Kampuni Bora ya Mawasiliano (Best Mobile Network Provider)
3. Mtumiaji Bora wa TEHAMA & Manufaa kwa Jamii
Swali la Muhimu ,ICT Commision alitumia vigezo gani kutoa tuzo hizo?
Je ni kweli Vodacom ,Airtel,Halotel na TTCL wako hoi wote mbele ya Tigo?
Kuna jambo lililo nyuma ya pazia ambalo muda sio mrefu litafumuka, inasemekana ,Uongozi wa ICT Commission waliomba ufadhili wa sherehe za utoaji tuzo hizo na Yas(Tigo) Ndio kampuni pekee ya simu iliyotoa Pesa kwa viongozi Binafsi sio Taasisi, inasemekana pesa taslimi Ambazo zilitoka Yas kufanikisha hilo zimeishia mifukoni mwa viongozi.
Waziri wa Sekta Jery Slaa alikuwepo kutoa tuzo hizo,waziri anaweza asijue undani wa vurugu hizi lakini makampuni ya Simu yasipimwe kwa kutoa fedha ili yapewe Tuzo, TCRA kila robo ya mwaka hua anatoa report zake ambazo kampuni kama ya Vodacom hua inaongoza kwenye maeneo kadhaa,Airtel maeneo kadhaa na Yas . Sasa ICT commissio wametumia taarifa zipi kutoa tuzo? wameendesha survey yeyote kwa wananchi? au walikaa kwenye vyumba vya ofisi zao wakapiga kura?
Waziri anapaswa kuwalinda watoa huduma za mawasiliano wote ,asiingizwe kwenye mtego wa wala rushwa wanaopewa pesa ili watoe tuzo kwa kampuni Moja