Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wako poa sana hawana majivuno, wanajiwekea mkazo katika kujifunza na sio kujigamba kwa upeo wao.
Wanatumia uzoefu kuyaangalia mambo na kuyachambua pia ili wafikie pale wanapopataka.
Hawashughulishwi na mambo madogo madogo ila wanabakia katika lengo lao husika
Wanafikiria kabla ya kutenda, wanatenga mda wa kutosha kutafakari mambo kabla ya kuyatatua.
Wanarahisisha mambo makubwa kuwa madogo ambayo yanaeleweka na rahisi kufanyiwa kazi
Huwa wanachagua maneno ya kusema mahala sahihi na kwa wakati sahihi
Ni watu wenye njaa na maarifa na kujifunza kila siku
Wanajifunza kwa kuangalia,huwa angalia wengine wanafanyaje kisha huwa na upeo mkubwa wa kufanya vizur zaidi
Hukifanyia kazi wanacho jifunza, tofauti na sisi wengine tunajifunza mambo lkn hatuyafanyii kazi
Huwa na tabia ya kuuliza maswali mengi ili wajifunze zaidi, sasa wewe mtoto wako akiwa anakuuliza maswali mengi unakereka,unaua kipaji cha mwanao huenda ana upeo mkubwa wa mambo
NI hayo tu!