Nenda Machinga Complex pale jengo la kwanza kama unaelekea kariakoo achana na lile la pili kama unaelekea boma au buguruni.
Pale Machinga Complex chini kabisa wala hupandishi kwenda juu/ngazi. Utakuta watu wa kutengeneza viatu, shanga na mambo mengineyo. Hapo ndo naona viatu vingi vya kimasai vinatengenezwa.
Ila quality ya kiatu itategemea na gharama. Wengi pale wanatengeneza viatu vya bei ya chini 5000, 7000, 8000 (bei za reja reja). Hapo wengine wanajumua na kuja kuuza mtaani 10,000, 12,000 unaweza uziwa hadi elfu 15 ukajuwa ni original.
Ila ukitaka kiatu original hapo inabidi uonane na fundi mwenyewe ukae naye chini myajenge.
Maana kiatu cha kimasai chenyewe original makamilisho yake kila kitu huwa inafika elfu 10,000 au zaidi kutegemeana na uwa au style ya kiatu chako, vile vile material yanayotumika (Ngozi, soli, sponji, karpet na nk).
Kwa uzoefu wangu rakini. Fanya uchunguzi wako pia ukifika pale au kwa mafundi wa viatu mtaani watakupa maelezo maana kalibia mafundi wengi wana chukulia baadhi ya vifaa hapo Machinga.