Vibali na Leseni za Uwekezaji kwa Ukanda Maalum wa Kiuchumi (SEZ)

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Leseni ya Mwendelezaji
Hii inatolewa kwa mwekezaji anayetaka kuwekeza katika miundo mbinu kama vile ujenzi wa majengo ya viwanda na maghala, ujenzi wa barabra za ndani, usawazishaji mazingira na ujenzi wa uzio pamoja na utoaji huduma za jamii kama vile nishati, maji, maji taka na mawasiliano.

Leseni ya Uendeshaji
Hii hutolewa kwa mwekezaji anayeendesha shughuli za uzalishaji katika ukanda huu malum (EPZ). Uendeshaji unaweza kuwa katika uzalishaji au uchakataji shughuli za biashara kama vile mwendeshaji kupunguza taka za malighafi, kuandaa vifungashio, uandikaji wa maandishi ya juu ya vifungashio, biashara, huduma zinazohusiana na biashara ya nje ya nchi pamoja na udalali, masuala ya habari na ushauri wa kitaalamu na huduma za matengenezo ya vitu mbalimbali.

Leseni ya Utoaji Huduma
Leseni hii hutolewa kwa wawekezaji wanaotaka kutoa huduma kwa kanda hizi maalum za kiuchumi. Wanaitwa watoa huduma na wanapewa leseni ya utoaji huduma kulingana na huduma watakazotoa kuanzia huduma za benki, bima, na Teknolojia ya habari na mawasiliano.

Taratibu za Kupata Leseni za Ukanda Maalum wa Uchumi (SEZ)

  • Mwekezaji anatakiwa kupeleka pendekezo la mradi katika ofisi za ukanda huu maalum wa kiuchumi (EPZA), kwa kujaza fomu za maombi na kukusanya mpango wa mradi na fomu ya maombi vyote kwa pamoja na ada isiyorudishwa kiasi cha dola za Marekani 250.
  • EPZA hutathmini mapendekezo ya mradi na kutoa barua ya maidhinisho kwa mwekezaji na kwa kawaida huchukua kati ya siku mbili mpaka tatu.
  • Mwekezaji anapata usajili wa kampuni ndani SEZ, halafu anapatiwa eneo/ardhi na kibali cha mazingira (pale kitakapohitajika).
  • Kwa maendeleo ya ukanda huu, EPZA huwezesha kupatikana kwa ardhi kutoka kwa Waziri wa Biashara na Viwanda.
  • Mwekezaji atatakiwa kulipa ada husika za leseni na hupewa leseni ya ukanda huu. Ada ya mwaka kwa mwenedelezaji wa SEZ ni dola za Marekani 5,000 wakati ada ya mtumiaji wa SEZ ni dola za Marekani 1,000 ambayo hulipwa ya kipindi cha miaka mitatu.
Baada ya taratibu hizo mwekezaji anaruhusiwa kuanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara alizozikusudia.Taratibu za Kupata Leseni za Ukanda Maalum wa Uchumi (SEZ)Mwekezaji anatakiwa kuulizia katika ofisi za ukanda huu EPZA kuhusu fursa ili kuthibitisha taratibu za uwekezaji, masharti ya uhakiki na uwezekano wa eneo la kiwanda au eneo la huduma

Kanuni zinazoongoza shughuli za EPZ na SEZ

Sheria ya Kanda Maalum ya Usafirishaji wa Bidhaa Nje (Export Processing Zone Act), 2012
Hii ni sheria inayopelekea uanzishaji, uendelezaji na uendeshaji wa Kanda hii maalum ya kiuchumi (EPZ) ili kuanzisha biashara za kimataifa kwa kukuza biashara ya nje na masuala yanayoendana na biashara katika ukanda huo. Sheria inaeleza kuhusu vivutio vinavyotolewa kwa wafanyabiashara katika kanda. Inatoa mamlaka na nguvu ya lutoa leseni na vibali Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uchumi (EPZA), na inaeleza masuala yote yanayoendana na biashara na shughuli zote katika ukanda huu (EPZ) (soma sheria yote).

Sheria ya Kanda Maalum za Kiuchumi (The Special Economic Zones Act (revised) ), 2012
Sheria hii ilipitishwa kwa ajili ya maendeleo na uendeshaji wa kanda maalum za uchumi ili kuanzisha mazingira ya kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ili kuwezesha kupanua ajira, kupata ukuaji uchumi na kutoa fursa zinazoambatana nayo (soma sheria yote).

Kanuni za Ukanda Maalum wa Kiuchumi (The Special Economic Zones Regulations), 2012
Hizi ni kanuni maalumu zinzotoa maelekezo ya namna ya kuendesha SEZ. Kanuni zinaeleza kuhusu taratibu mbali mbali na masharti anayotakiwa mtu kujihusisha na shughuli za biashara za SEZ.

Pia zinatoa taarifa kwa makosa na faini kwa atakayeendesha shughuli ndani ya kanda bila leseni maalumu (soma kanuni zote).

Chanzo: FURSA ZA UWEKEZAJI | MSMEs Information Portal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…