Vibali vya kazi vya wazungu wa tanzaniteone vyachunguzwa

Vibali vya kazi vya wazungu wa tanzaniteone vyachunguzwa

mzalendo2013

New Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
1
Reaction score
1
Wakuu nimepata taarifa za ndani ya kampuni ya uchimbaji wa Tanzanite, Tanzaniteone iliyopo Mererani kuwa watu toka idara ya uhamiaji wameenda kwa uchunguzi wa vibali vya wanaojidai ni ma expert. Taarifa zinasema wamekuta wengi wao hawana vibali na hawana sifa kufanya kazi nchini.

Wengi wao walikuwa wakipatiwa vibali vya mda kijanjajanja na wahusika serikalini ilhali wakijua hawana sifa kabisa kufanya kazi nchini akiwemo general meneja kwa malipo ya fedha, kupatiwa ajira ndugu zao, kupewa viroba si vya pombe ila ni vile ambavyo vina tanzanite reject. Wanaotuhumiwa kwenye hili ni baadhi ya mawaziri akiwamo wa kazi na ajira, baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya, kamishna wa sasa wa madini na aliyemtangulia, watumishi kutoka uhamiaji, tume ya uwekezaji, wizara ya kazi na maendeleo ya vijana nk. Wote hawa wanafanya haya yote kwa maslahi yao binafsi na kuidhoofisha taifa na mwananchi wa kawaida.

Kwa mzingira haya naona kuna haja sasa( ingawa tulichelewa) ya kuangalia rasilimali hii peke kuangaliwa kwa jicho la peke kwani inaonyesha kuwa wawekezaji uchwara wanashirikiana na watumishi wa serikali kuiibia nchi rasilimali hii toka inavyo chimbwa, inavyothaminishwa na kusafirishwa ni utata mtupu.

Hata kwenye huu uchunguzi bado nina walakini na hatima yake kwani watumishi wa hizi idara ni walewale na kwa utendaji ulele, sitegemei matokeo tofauti zaidi ya kuendelea kutonesha kidonda hiki kibichi. Natumai mwisho wake utakuwa wa kupeana bahasha na ahadi kekem toka kwa watetewa kuneemesha nafsi chache. Hivyo katika hili wazelendo wa nchi hii tuweze kusimama imara kuchunguza na kutokomeza wezi wa rasilimali zetu kwa manufaa ya nchi na vizazi vijavyo ingawa na imani mambo ni haya haya kwenye rasilimali nyingine mfano wanyama pori nk.

Hivi karibuni nimesikia na kuona kwenye tangazo la serikali la tarehe 2/5/2013 kwenye gazeti mojawapo lilotolewa na wizara ya nishati na madini kuwa STAMICO kwa kushirikiana kwenye nyanja zote kwa 50% kila moja na kampuni ya Tanzaniteone kuchimba haya madini ya vito. Wasiwasi wangu katika hili ni juu ya umakini wa serikali katika uwekezaji wa pamoja kama ilivyotokea kwa Celtel, BP, ATC, TRC, STARTIMES nk. Tumeshuhudia haya yote kwa macho yetu na matokeo yake, kila aliye kwenye systeam ingawa si wote anabomoa nchi katika pembe anayoona inafaa. Sina hakika kama serikali imefanya utafiti wa kina kuhusu reserve iliyobakia pale Block C kwani haya makaburu yalishachimba kwa mda mrefu, nashangaa serikali ina rush kama FASTJET kwenye vitu ambavyo vinahitaji uchunguzi wa kina kwa kushirikisha wataalamu wazalendo wa ndani na nje kama watahitajika, naimani wapo ambao wanafanya kazi pale.
Hii tabia ya kukurupuka na kukumbuka shuka wakati mawio yalishajiri sijui nchii itaisha lini.

MABADILIKO YANAWEZEKANA NI SISI TWAWEZA.

Nimetoa angalizo tu wakuu, kwa pamoja tutafika.
 
Back
Top Bottom