The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema ndoa nyingi za watumishi wa umma zinakufa kutokana na wenza kukaa mbalimbali na kwamba wiki ijayo vitatolewa vibali zaidi ya 200 ili wasogezwe na familia zao.

Akifungua leo kikao kazi kati yake na Wakuu wa Taasisi za Umma, Simbachawene amesema “Wapo watumishi ambao tangu ameanza kazi ndoa ina miaka 20 hajawahi kukaa na mume wake kwa zaidi ya mwezi mmoja, wewe Mkurugenzi hasa wa Halmashauri unamzuia huyu kutekeleza ombi lake la uhamisho, wewe unajua kabisa amekaa miaka 20 pale, hata anapokaribia kustaafu busara zikuongoze inahitajika huruma naye akajenge familia yake.”
Amesema amezungumza hilo mara nyingi kwa kuwa amebeba uhusika wa mzazi na kwamba binti anapokaa mbali na mume wake inaathiri hadi malezi ya watoto.
“Kuna mwingine anaona anakaribia kustaafu anaona kikokotoo chake kidogo anaomba ahamishwe karibu na nyumbani, hiyo busara haikupati unaona upo sawa, niwaombe mtumie busara kwenye hili,”amesema.
Ameomba waongozwe na busara kwenye suala la uhamisho kwa kuwa wataokoa mambo mengi kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
“Tumejipanga sisi tutatoa wale ambao mchujo umekamilika kama zaidi ya 200, wiki ijayo muwasiliane na TAMISEMI mnapopokea ajira mpya mna nafasi ya kuziba mapengo ya uhamisho wa watumishi ambao watakuwa wamekwenda kusogea na familia zao lakini takribani 20,000 mmekaa nazo, nawaomba mtumie busara muokoe ustawi wa familia hizi,”amesema.