Vibanda 15 vyateketea kwa moto Mafinga

Vibanda 15 vyateketea kwa moto Mafinga

John7371

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
2,994
Reaction score
6,676
Mufindi. Moto umezuka saa saba usiku wa kuamkia leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 pembezoni mwa Soko la Mafinga Mjini Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na kuteketeza vibanda 15 na mali za wafanyabiashara.

Akizungumza na Mwananchi mmiliki na shuhuda, Mohamed Migila amesema kuwa moto huo ulianza kuwaka usiku na mali nyingi zimeteketea kutokana na shughuli ya uokoaji kuwa mgumu baada ya moto kusambaa kwenye vibanda hivyo.

"Baada ya moto kuwaka, tulifanya jitihada mbalimbali kwa ajili ya kuokoa mali za wafanyabiashara hao lakini hatujafanikiwa baada ya moto kusambaa kwenye vibanda hivyo," amesema Migila.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Iringa, SF Isabela Mbwago amethibisha kutokea kwa moto huku akisema thamani ya mali ambazo zimeteketea bado haijafahamika.

Source- Mwananchi
 
Kwenye hizi zama vibanda vinapata tabu kwelikweli. Ifike mahala hawa watu wawe na huruma kwa binadamu wenzao.
 
Back
Top Bottom