DOKEZO Vibanda na makontena maeneo ya Urafiki (Dar) yanatumika kama danguro na Watumiaji wanajisaidia ovyo

DOKEZO Vibanda na makontena maeneo ya Urafiki (Dar) yanatumika kama danguro na Watumiaji wanajisaidia ovyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Hapa kwenye nyumba za Shirika la Nyumba NHC maeneo ya Urafiki karibia na Shekilango inasikitisha kuona kuna vibanda na makontena yamezagaa na kuzunguka nyumba za shirika hilo huku baadhi yakitumiwa na Vijana kufanya kama madanguro.

Baadhi ya Makontena hayo hayana huduma muhimu kama choo lakini Watu wamekuwa wakiyatumia kulala humo ndani pia.

Kontena na mabanda hayo yapo karibu na Kituo cha Polisi cha Urafiki na maeneo ya karibu, kimsingi yamewekwa mbele ya majengo ya ghorofa za NHC, hivyo kuwa kero kwa ofisi na wakazi waliopangishwa rasmi kwenye nyumba hizo.
photo_2024-12-03_12-04-07 (2).jpg

photo_2024-12-03_12-04-06.jpg

Hali hiyo imesababisha adha kwa wapangaji na wafanyabishara wa ofisi za majengo haya. Tunaomba Halmashauri ya Jiji na mipango miji wafanye utaratibu tena wa haraka iwezekanavyo, kwani wamiliki na wateja wa vibanda bubu hivi na kontena zinatumia maeneo ya nyuma yake kujisaidia kwa kuwa hayana vyoo, jambo ambalo ni hatari kwa afya.

photo_2024-12-03_12-04-07.jpg
 
Siyo kwenye kontena tu Hadi kwenye nyumba za shirika na kituo Cha polisi kimegeuzwa kuwa danguro usiku
 
Back
Top Bottom